Saturday, March 4, 2017

WANAFUNZI WAUGUZI WA CHUO KIKUU CHA WRIGHT, JIMBO LA UHAYO MAREKANI WATEMBELEA SKULI YA AFYA NA SAYANSI ZA TIBA YA SUZA MBWENI.

1
Kaimu Mkuu wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Amina Abdulkadir akizungumza na wanafunzi wauguzi wa Chuo Kikuu cha Wright Jimbo la Ohayo nchini Marekani walipotembelea Skuli hiyo Mbweni  kubadilishana uzoefu.
2
Mwanafunzi Muuguzi kutoka Chuo Kikuu cha Wright nchini Marekani Melissa Vanscoy akieleza lengo la ziara yao hapa Zanzibar  wakati wanafunzi wa vyuo hivyo viwili walipokutana katika Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya SUZA Mbweni.3
Wanafunzi wauguzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya SUZA  wakibadilishana mawazo na wanafunzi wenzao wa Chuo Kikuu cha Wright kutoka Jimbo la Uhayo Marekani walipowatembelea skulini kwao Mbweni.
4
Wanafunzi wauguzi kutoka Chuo Kikuu cha Wright na SUZA wakiwa katika darasa la kufanyia mazoezi ya vitendo wakielekezana namna ya kumuhudumia mgonjwa alielezwa wodini.
5
Picha ya pamoja ya wanafunzi wauguzi wa Skuli ya Afya na Sayansi za Tiba ya SUZA wakiwa na baadhi ya walimu  na wenzao wa Chuo Kikuu cha Wright, Jimbo la Uhayo nchini Marekani wakiwa katika kempasi ya Mbweni.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

No comments: