Saturday, March 4, 2017

SHILINGI MILIONI 10.8 ZAKUSANYWA KATIKA VITA YA UVUVI HARAMU GEIT

Mkuu wa Mkoa wa GeitaMeja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga akiteketeza
dhana haramu ambazo zimekamatwa katika oparation iliyofanyika kwenye
mialo iliyopo Mkoani Geita lengo likiwa ni kutokomeza uvuvi haramu ambao
umeendelea kwa kasi kwenye mialo ya Izumacheli na Mganza.
Baadhi ya wananchi wakivuta kokolo wakipeleka eneo la kuchomea.
Dhana haramu za uvuvi zikiwa zimekusanywa kwaajili ya kuchomwa kwenye
mwalo wa dala dala uliopo kijiji cha Nyasalala kata ya Bukondo.
Katibu wa BMU mtandao wa kata ya Bukondo Methusela Samweli akisoma
Risala ambayo ilikuwa inaelezea changamoto ambazo wamekuwa wakikutana nazo
katika utendaji kazi wao wa kila siku wa kutokomeza uvuvi haramu.
Meza kuu ikongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita ,wakisiliza kwa makini
taarifa ambayo ilikuwa ikisomwa na afisa uvuvi.
Afisa
mfawidhi udhibiti ubora wa samaki na usimamizi wa rasilima za uvuvi
kanda ya Mkoa wa Geita Shafii Ramadhan Kiteri,akitoa taarifa ya zoezi la
oparesheni Tokomeza uvuvi haramu.

Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Geita,Bi Janneth Mobe akimkaribisha Mkuu
wa Mkoa kuzungumza na wananchi wa kijiji cha Nyasalala.
Mkuu wa Mkoa wa GeitaMeja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga,akizungumza
na wananchi wa kijiji cha nyasalala juu ya wao kutoa ushirikiano kwa serikali
katika kupambana na uvuvi haramu.
Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Geita wakati alipokuwa
akizungumza.
Afisa mfawidhi udhibiti ubora wa samaki na
usimamizi wa rasilima za uvuvi kanda ya Mkoa wa Geita Shafii
Ramadhan Kiteri,akimwonesha mkuu wa Mkoa nyavu aina ya dududu ambazo zimekuwa
zikitumika kuvulia samaki ambao wanakuwa bado awajafikia muda wa kuvuliwa.


Zoezi la uchomaji wa dhana hizo za uvuvi likiendelea.
Wito umetolewa kwa wananchi ambao wanafanya shughuli za uvuvi Mkoani Geita,kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali kwa kuwafichua wale ambao wamekuwa wakijihusisha na shughuli ya uvuvi haramu katika mialo iliyopo Mkoani Humo.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga wakati wa zoezi la kuteketeza zana haramu za uvuvi kwenye Mwalo wa daladala uliopo kijiji cha Nyasalala kata ya Bukondo zilizokusanywa ndani ya miezi miwili kuanzia Januari hadi Februari mwaka huu.

Aidha mh Kyunga amesema kuwa uhifadhi wa rasilimali zilizopo kwenye ziwa viktoria ni muhimu kwa kila mwananchi kwani endapo
uvuvi haramu ukiachiwa madhara yake yanaweza kuwa ni makubwa kwa viumbe ambavyo vipo katika ziwa.

“Ndugu wananchi kwa kweli uhifadhi rasilimali zilizomo katika ziwa letu hili ni muhimu ,ni muhimu kwa sasa na vile vile kwa baadae isipokuwa mimi nisisitize sisi wote hapa kwa ajili ya ustawi wetu na vizazi vijavyo tuone kwamba tuna wajibu wa kuhifadhi mazingira na matumizi bora ya ziwa letu hili,tukilivuruga kama hawa wenzetu wanavyolifuruga kwa kuendesha uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira hasara ambayo wanatuachini ni kubwa sana hawa watu kwa lugha nyingine naweza kusema ni wachawi”Alisema Kyunga

Hata hivyo katibu wa BMU mwalo wa Daladala,Methusela Samweli amemweleza Mkuu wa Mkoa kuwa changamoto kubwa ambayo wanapambana nazo katika zoezi la kutokomeza uvuvi haramu ni
kukosekana kwa vitendea kazi ikiwemo kukosekana kwa Boti kutokuwepo kwa ulinzi wa kutosha ambao utasaidia usalama wakati wa doria.

Karoli Makoba na Baraka Mkwazu ni wananchi ambao
wapo kwenye mwalo huo wameiomba serikali na BMU kuweka uhusiano wa karibu kwa kushirikiano hili kutokomeza tatizo la uvuvi haramu ambalo limeendelea kushamiri kwa kasi kubwa hususani kwenye mialo ya Izumacheli na Mganza.

Kwa mujibu wa maelezo ya afisa mfawidhi udhibiti ubora wa samaki na usimamizi wa rasilima za uvuvi kanda ya Mkoa wa Geita Shafii Ramadhan Kiteri,ameelezea kuwa Doria ambayo imefanyika kwa miezi miwili imefanikisha kukamata jumla ya samaki wachanga ambao Kg 7,682,Mitumbwi 19,watuhumiwa 12,gari moja Hiace na Gari ya pili aina ya Fuso Tandam,pikipiki 3,Nyavu za makila 1,261,Makokoro
ya kuvutwa nchi kavu 23,Dududu 41na Timba 17.

Kiteri ameongezea kuwa Katika doria hizo
zote kiasi cha shilingi Milion,10,080,000 zimepatikana ambazo zimetokana
na faini mbali mbali ambazo walikuwa wakilipa watuhumiwa .

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE BLOG

No comments: