Thursday, March 2, 2017

VIONGOZI WA MIKOA NA WILAYA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA USHIRIKIANO KUIBUA FURSA ZA UWEKEZAJI NCHINI


Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

VIONGOZI wa Mikoa na Wilaya wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano katika kuibua fursa za uwekezaji na kuibua miradi itakayo wawezesha Wananchi kunufaika na ukuaji Wa uchumi katika kuelekea kuwa Nchi ya viwanda ilikuwawezesha Wananchi kuepukana na umasikini .

Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora , Agrey Mwanry ambae pia ni mwenyekiti wa Baraza la uwezeshaji kanda ya ziwa Mkoani kigoma katika Semina ya mafunzo ya uwezeshaji kwa Viongozi wa Mikoa na Wilaya za Kigoma, Kagera , Tabora na Katavi ya kanda ya Mgharibi ambayo iliandaliwa na Baraza la uwezeshaji Taifa iliyo lenga kuwawezesha viongozi kuwajengea uwezo wananchi katika kukuza uchumi.

Mkuu huyo alisema ilikuwawezesha Wananchi kunufaika na uchumi ni lazima Viongozi kushirikiana katika kuibua Fursa za uwekezaji na kuboresha Miundombinu itakayo saidia Wananchi kunufaika na uchumi katika kufanya shughuri zao katika mazingira mazuri na yanayo wavutia katika kuboresha uthamani wa bidhaa Wanazo zalisha.

Mwanry alisema Viongozi kazi yao kubwa ni kuonyesha njia ya maendeleo kwa Wananchi juu ya ukuaji wa kiuchumi, fursa zinazotakiwa kuibuliwa ni pamoja na kila halmashauri kutenga bajeti ya maendeleo ya wananchi kwa Asilimia tano ilikuweza kuwawezesha Wananchi kuepukana na umasikini na kunufaika na Ukiaji wa uchumi.

"Mimi kwa upande wangu katika Mkoa wa Tabora kitendo cha baadhi ya viongozi wa Wilaya na Wakurugenzi kuwa miongoni mwa walalamikaji dhidi ya kero zinazo wakabiri Wananchi na kushindwa kuzitatua ni kutotambua nafasi zao katika jamii , kwa upande wa Mkoa wa Tabora siwezi kukubari kupitisha bajeti za Halmashauri ambayo haitatenga asilimia tano ya bajeti yake kwaajili ya fedha za maendeleo ya Wananchi ni tatizo kubwa katika kudidimiza uchumi kwa Wananchi.

Kwa upande wake katibu mtendaji baraza la uwezeshaji Taifa , Beng'i Issa alisema lengo ni kuwawezesha Viongozi kutambua majukumu yao kushirikiana na Wadau wa maendeleo kuwawezesha Wananchi katika fursa za maendeleo pamoja na kuboresha miundombinu itakayo saidia kukuza uchumi katika maeneo yao.

Alisema semina hiyo itawasaidia viongozi kuweza kuibua fursa mbalimbali za kiuchumi katika kuwawezesha Wananchi kujishughurisha katika biashara mbalimbali na kuinua uchumi Wa Wananchi wa kipato cha chini hadi serikali ilikuwezesha na Wananchi kunufaika na uchumi huo.

Beng'i alisema kigezo kinacho tumika kupima ukuaji wa uchumi ni jinsi Maisha ya wananchi wa eneo husika yalivyo badilika katika pato lao kiuchumi pamaja na maisha wanayo ishi kwa ujumla endapo Mkoa utafanikisha masuala hayo itakuwa imefikia lengo hilo.

No comments: