Monday, March 20, 2017

SOKO LA MBAO LIMESHUKA WILAYANI MUFINDI

Mbunge wa mafinga mjini Cosato Chumi akiongea na Wafanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Mufindi juu ya malamiko yao kwa TRA mkoa wa Iringa
Baadhi ya wafanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Mufindi waliohudhulia mkutano wa pamoja kati ya mbunge,TRA na wafanyabiashara.


Na Fredy Mgunda,Mufindi 

Wafanyabiashara wa mazao ya misitu wilayani Mufindi wamesema kuwa soko la mbao limeshuka kwa kiwango kikubwa kutoka na mrundikano wa kodi katika wilaya hiyo tofauti na wilaya nyingime.

“Ukienda mbeya,njombe na maeneo mengine kodi ya vibali ni ndogo kuliko ya hapa mufindi sasa tunataka kujua tatizo nini”walisema wafanyabiashara

Aidha wafanyabiasha hao wameiomba mamlaka ya mapato mkoa wa iringa TRA kutoa kibali cha usafirishaji kwa kuondoa usumbufu wa tozo za ushuru check point na kuombwa lisiti za mashine kutoka kwa wakulima waliowauzia mbao na nguzo.

Akizungumza mmoja wa wafanyabiashara hao Zakayo Kenyatta Katika mkutano wa wafanyabiashara wa mazao ya misitu na TRA alisema kuwa TRA wamekuwa wasumbufu sana check point kwa kuwasimamisha zaidi ya siku tatu wakidai lisiti hizo huku wafanyabiashara wakionyesha barua za watendaji kutoka vijiji walivyonunulia zikikataliwa.

"Tunawaomba TRA mkatoe elimu kwa mkulima mmoja mmoja kwa sababu ni ngumu sana mkulima wa chini akuulizie nguzo 5 alafu awe na lisiti ya mashine kwa hiyo tunawaomba TRA wakatoe elimu hiyo na kuwaamasisha wakulima hawa Kuwa na hizo mashine kwani wakulima hao ni wale ambao wanauza miti yako kutokana na matatizo mbali mbali walionayo na sio kampuni" alisema Kenyatta

Akijibu hoja hiyo meneja msaidizi WA TRA mkoa WA iringa Mustapha Mkilamwenye alisema Kuwa wamekuwa wakiogopa kwenda kutoa elimu hizo kwa wakulima kutokana na mkutano yao kuharibika kwa kuzomewa na kutokufikia muafaka WA uelimishaji.

Pia Mkilamwenye amewataka wafanyabiashara hao kupata kibari cha kununua na kusafirisha kutoka TRA wilaya au mkoa kabla hqwqjaenda vijijini kununua ili kukwepa uwumbufu huo check point.

"Ombi lenu tumelipokea hivyo tunawaomba kabla hamjanunua mpate kibali kutoka TRA mkoa au wilayani kuokoa usumbufu WA tozo za ushuru check point, pia tutatoa elimu ya matumizi ya mashine kwa wakulima vijijini wauzapo miti yako kwa wafanyabiashara" alisema

Kwa upande wake Mbunge wa mafinga mjini Cosato Chumi alisema Kuwa ameamua kuwakutanisha wafanyabiashara na TRA kupata ufafanuzi WA kuombwa ushuru check point kutokana na kulalamikiwa na wafanyabiashara hao Kuwa magari yako wamekuwa wakikaa check point zaidi ya siku tatu wakiombwa lisiti za mashine kutoka kwa wakulima waliowauzia nguzo na mbao.

"Mkutano huku ni mahususi kwa wrote tukipata ufafanuzi na kujua kwa nini mnakamatwa check point na mkiobwa ushuru au njia kila mkoa,tra wanapaswa Kuwa rafiki Wa wafanyabiashara na sio adui kwa sababu mufindi ndio chanzo kikuu cha mapato ya nchi kutokana na zao LA mbao" alisema Chumi

Meneja wa TRA wilayani ya Mufindi Filmoni Mwakapesile alisema Kuwa "ni kweli tuhuma hizo na lawama tumezipata na tumekuwa tukipokea simu nyingi za wafanyabiashara na kutatua matatizo yako lakini Leo tunashukuru Mbunge amekututanisha na tumewapa uelewa na sisi kama TRA tumewaambia mini cha kufanya kuondoa huo usumbufu"

No comments: