Monday, March 20, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

SIMU.TV: Rais Dr. John Pombe Magufuli ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara za juu eneo la Ubungo jijini Dar es Salaam na kuwataka watanzania kutopoteza muda kwa mambo yasiyo na tija. https://youtu.be/FhLQdhNhrAo

SIMU.TV: Rais Dr John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na rais wa benki ya dunia Dr Jim Yong Kim ikulu jijini Dra es Salaam. https://youtu.be/YffVjTJP3Zg

SIMU.TV: Waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Nape  Moses Nauye amelaani uvamizi unaodaiwa kufanywa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam  katika kituo cha habari cha Clouds Media. https://youtu.be/SbBjjGUNudw

SIMU.TV: Kampuni hodhi ya rasilimali za reli RAHACO imesema zoezi la bomoa bomoa kupisha mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa unazingatia sheria na taratibu. https://youtu.be/HeieInlallA

SIMU.TV: Kukosekana kwa miundombinu rafiki ya kutolea elimu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu imetajwa kuwa changamoto inasababisha kutofikia malengo yaliyokusudiwa katika kutoa elimu maalumu kwenye shule ya msingi Utegi wilayani Rorya. https://youtu.be/RD-cPBmXW_4

SIMU.TV: Walimu wa shule ya msingi maalumu ya wasioona ya Malangali mkoani Rukwa wameiomba serikali kuwaingiza wanafunzi wa shule hiyo katika mfumo wa bima ya afya ili waweze kupata huduma za afya kwa uraisi zaidi. https://youtu.be/21kxJUl6ZB8

SIMU.TV: Rais wa benki ya dunia Dr Jim Yong Kim amesema maendeleo ya nchi kiuchumi hayawezi kupatikana kama hakuna uwekezaji wa kutosha katika elimu. https://youtu.be/LgLmSVTBy6Y

SIMU.TV: Wafanyabiashara nchini wanatarajia kukuza soko la bidhaa zao nchini Mauritius baada ya jumuiya ya wafanyabiashara nchini kukutana na wafanyabiashara kutoka nchini humo kujadili kuhusu masoko kwa nchi hizo mbili. https://youtu.be/BwNmE7k3S7A

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Singida Dr Rehema Nchini amesema jitihada zinazofanywa na serikali katika kuwainua wakulima hazitazaa matunda kama watendaji wa vyama vya ushirika hawatabadilika katika utendaji wao. https://youtu.be/xXWjWsTLbTw

SIMU.TV: Wananchi wa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya wanao nufaika na mpango wa TASAF wameeleza kupata faida nyingi kupitia mpango huo ikiwemo kumudu gharama za maisha. https://youtu.be/o-kdLG_PNng

SIMU.TV: Timu ya taifa ya vijana ya Serengeti Boys imeendelea na mazoezi kwenye viwanja vya Jakaya Kikwete ikiwa ni maandalizi awamu ya kwanza katika kuelekea nchini Gabon kwa ajili ya fainali za kombe la vijana barani Afrika. https://youtu.be/hFCp9b4wSLs

SIMU.TV: Mpinzani wa Yanga katika michuano ya kombe la shirikisho hatua ya makundi barani Afrika anatarajiwa kujulikana kesho kwenye droo itakayochezwa mjini Cairo nchini Misri. https://youtu.be/9iPL3TNIp2g

SIMU.TV: Klabu ya soka ya Arsenal imekanusha taarifa zilizoenea mitandaoni kuwa imeaanza mchakato wa kumtafuta mbadala wa kocha Arsene Wenger. https://youtu.be/kHLqI_ZHy4g

No comments: