Friday, March 24, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Rais Dr John Pombe Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam ili kuona utekelezaji wa maagizo aliyo yatoa. https://youtu.be/pH4EtD4G2VA

SIMU.TV: Mkutano wa waandishi wa habari ulioandaliwa na aliyekuwa waziri wa habari sanaa na michezo Nape Nauye umeingia dosari baada ya kuahirishwa na baadae kufanyika katika eneo la wazi. https://youtu.be/TGN7d15_7G4  

SIMU.TV: Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe imetoa idadi ya vijiji ishirini na nne kwa ajili ya jamii ya wafugaji wilayani humo. https://youtu.be/lVBGd_LbqLg

SIMU.TV: Wizara ya ujenzi uchukuzi na mawasiliano imeitaka bodi ya wakadiriaji na wabunifu wa majenzi kuwachukulia hatua wakadiriaji majenzi na wahandisi wazembe wanaokiuka sheria na kuhatarisha maisha ya wananchi. https://youtu.be/vftJ8GzMggM

SIMU.TV: Mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA leo imeungana na mamlaka kama hizo duniani kuadhimisha siku ya hali ya hewa duniani. https://youtu.be/pLDLAkfFZKY

SIMU.TV: Jeshi la polisi mkoani Rukwa limekamata shamba la zao la mahindi lililochanganywa na mimea ya bangi katika kijiji cha Mawenzusi. https://youtu.be/GXYC_iyUpzc

SIMU.TV: Mabalozi wa Tanzania nchini Kenya Uganda na Qatar wamesema wataitumia nafasi yao ya uwakilishi kuitangaza Tanzania ili iweze kupata wawekezaji nakufikia azma ya uchumi wa viwanda. https://youtu.be/ZRxFjy77cUM

SIMU.TV: Shirika la viwango Tanzania TBS limeendelea na ukaguzi wa bidhaa jijini Dar es Salaam na kukamata bidhaa mbalimbali vikiwepo vilainishi na kuziteketeza. https://youtu.be/zdc6h8dhnH8

SIMU.TV: Shirika la nyumba la taifa NHC limeshauriwa kujenga nyumba za bei nafuu zaidi ili kila mtanzania aweze kununua nyumba. https://youtu.be/FU8JtXLOeSo

SIMU.TV: Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ujerumani Lucas Podolsk ameipa ushindi timu yake ya Ujerumani jana usiku baada ya kufungia bao la pekee kwenye mchezo wao dhidi ya Uingereza. https://youtu.be/F6bYZlVqI6M

SIMU.TV: Chama cha mpira wa miguu wilayani Hanang kimesema ukosefu wa viwanja, waamuzi wanaojua sheria na makocha wenye viwango ni kati ya changamoto zinazokwamisha maendeleo ya mchezo wa soka wilayani humo. https://youtu.be/i_8JFE1uhJE

SIMU.TV: Kituo cha mazoezi ya viungo cha Power of Fitness kimeandaa tamasha la mazoezi siku ya jumamosi ya wiki hii katika viwanja vya posta jijini Dar es Salaam ambapo hakutakua na kiingilio. https://youtu.be/rtAyY_bLVJ4

No comments: