Thursday, March 23, 2017

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddiatembelea kampuni ya Mahindra jijini New Delhi, India


Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi katika utengenezaji wa vyombo vya Moto ya Mahindra yenye Makao Makuu yake Mjini New Delhi Nchini India imeamua kuiunga Mkono Zanzibar katika muelekeo wake wa kuimarisha miradi ya maendelelo. 
Mkuu wa shughuli za Kimataifa wa Kampuni hiyo Bwana Arvind Mathew alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha pamoja kati ya Uongozi wa Kampuni yake na Ujumbe wa Zanzibar unaoongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kilichofanyika Makao Makuu ya Kampuni hiyo yaliyopo Mjini New Delhi. 
Bwana Arvind Mathew alisema kutokana na kukuwa kwa Teknolojia ndani ya Kamupuni ya Mahindra, Uongozi wa Taasisi hiyo ya Uhandisi Nchini India hivi sasa umekusudia kuelekeza nguvu zake katika Mataifa rafiki kwa nia thabiti ya kuona Mataifa hayo hasa yale ya Bara la Afrika yanakuwa Kiuchumi. 
Alisema Mahindra imejipanga kuangalia njia za kusaidia uimarishaji wa Sekta ya Kilimo kupitia miundombinu imara na vifaa vya Kisasa vitakavyoongeza nguvu za uzalishaji kwa kundi kubwa la Wakulima katika mazao ya viungo yenye tija kubwa katika soko la Kitaifa na Kimataifa. 
Alisema Wataalamu wa Kampuni ya Mahindra wamekuwa shahidi katika safari zao za kawaida kwenye Mataifa mbali mbali waliyowekeza miradi yao ya Kiuchumi kuwaona Wakulima wa maeneo hayo wakiendesha shughuli zao katika mazingira magumu. 
Bwana Arvind Mathew alieleza kwamba wakulima wengi hasa katika Nchi changa zinazojikita kuendelea wamekosa Taaluma ya kutosha katika kuimarisha Kilimo chao jambo ambalo wanadiriki kupata kipato kidogo huku wakitumia nguvu nyingi zaidi wakati wa uzalishaji. 
Naye Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Biashara cha Kampuni ya Mahindra Kanda ya Afrika Bwana Saurabh Kohli aliueleza Ujumbe wa Zanzibar ulio mwishoni mwa ziara yake Nchini India kwamba Mahindra imekusudia kuwa na Mtandao wa Kimataifa katika mfumo wa Uzalishaji katika Nchi mbali mbali walizowekeza Ulimwenguni. 
Bwana Saurabh Kohli alisema Mahindra iliyoasisiwa kwama 1945 ikianza na uzalishaji wa gari aina ya Jeep kwa sasa tayari imeshawekeza katika Mataifa Mia Moja kwenye nchi mbali mbali Duniani ikiwa na wafanyakazi wasiopungua Laki 200,000 ikianza na mtaji wa Dola za Kimarekani U$ Bilioni 16.5. 
Akitoa shukrani kwa niaba ya ujumbe wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Seif alisema ushirikiano wa karibu uliopo kati ya Zanzibar na Kampuni ya Mahindra umetoa mchango mkubwa katika kuwakomboa Wananchi na hasa Wakulima wa Zanzibar. 
Alisema Wananhi wa Zanzibar zaidi ya asilimia 70 walioko Vijijini katika Visiwa vya Unguja na Pemba wanaendesha maisha yao ya kila siku kwa kutegemea sekta ya Kilimo. Wakati huo huo Ujumbe wa Zanzibar ulikutana kwa mazungumzo na Wawekezaji pamoja na Wafanyabiashara tofauti wa Mji wa New Delhi na Majimbo jirani yanayouzunguuka Mji huo yaliyofanyika Makamo Makuu ya Shirikisho la Viwanda la India { CII }. 
Katika mazungumao yao Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirikisho hilo ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ushauri wa Kimataifa wa CII Bwana K.K Kapila alisema India na Tanzania ikiwemo Zanzibar kwa ujumla zimekuwa na ushirikiano wa karibu wa Kibiashara uliotiwa saini mnamo mwaka 1974. 
Bwana Kapila alisema ushirikikano huo unaoendelea kuimarika kila siku umeibuwa mchango mkubwa wa msaada wa fedha zitakazosaidia uimarishaji wa huduma za Maji safi na salama katika Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar kufuatia ziara ya mwaka jana ya Uongozi wa ngazi ya juu ya India uliofika Tanzania Mwezi Disemba mwaka 2015. 
“ Uwepo wa wafanyakazi zaidi ya 10,000 wanaotoka Nchini India wakifanya kazi Tanzania na Zanzibar kwa ujumla ni uthibitisho wa ushirikiano uliopo kati ya pande hizo mbili. 
Naye kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Zanzibar imeshafungua milango ya uwekezaji kwa makampuni mbali mbali ndani na nje ya Nchini tokea miaka ya 90. 
Alisema zipo sekta ambazo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshazijengea uwezo kwenye miundombinu itakayotoa wepesi kwa Taasisi pamoja na Makampuni yenye nia na maamuzi ya kutaka kuwekeza miradi yao ya Kiuchumi Visiwani Zanziobar. 
Balozi Seif aliitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa inapatikana katika sekta ya Afya, Kilimo, Miundombinu, Elimu pamoja na sekta isiyo ya kiserikali inayotoa ajira kubwa zaidi kwa makundi ya akina mama na Vijana.

No comments: