Wednesday, March 8, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Wakazi wa mabondeni hususani maeneo ya Msimbazi na Kigogo jijini Dar es Salaam wamelazimika kuzikimbia nyumba zao baada ya kujaa maji kutokana na mvua iliyonyesha leo asubuhi. https://youtu.be/iCXzYEOmKrg

SIMU.TV: Msafara wa kamati ya kudumu ya bunge ya ardhi maliasili na utalii jana ulikumbana na wakati mgumu baada ya wananchi wa Loliondo kulala barabarani wakiuzuia ili kueleza kero zao. https://youtu.be/AI8Pb3wLMx8

SIMU.TV: Waziri mkuu Kasim Majaliwa anatarajiwa kufungua mkutano wa wadau wa mfuko wa hifadhi ya jamii wa LAPF utakaofanyika March 9 jijini Arusha. https://youtu.be/9tmKACYMspc

SIMU.TV: Tanzania imeungana na nchi nyingine duniani katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambapo serikali imehimizwa kuwajengea wanawake mazingira rafiki ya ulipaji kodi. https://youtu.be/mYrAiMP5Ci4

SIMU.TV: Waziri wa nchi ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Angela Kairuki ameongoza akina mama wa UWT wilaya ya Ilala kutoa misaada mbalimbali katika hospitali ya taifa ya Muhimbili. https://youtu.be/YEFKo0AR9s0

SIMU.TV: Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania limeshauriwa kutenga bajeti ya kuendeleza viwanda vidogo hapa nchini ili kuwainua wanawake wajasiriamali kiuchumi. https://youtu.be/UudkbKFDCao

SIMU.TV: Kampuni ya Mihani Gas imekabidhi zawadi ya mtungi wa gesi kwa mshindi wa kampeni ya kuzipa thamani kazi duni zinazofanywa na wanawake. https://youtu.be/c-EGXJ0o_do

SIMU.TV: Ufinyu wa idadi ya wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi umetajwa kuwa changamoto inayo kwamisha jitihada za kumkomboa mwanamke. https://youtu.be/Y_GA6h_IbHk

SIMU.TV: Sekta ya kilimo imeelezwa kuwa ndio nguzo muhimu katika kuifanya Tanzania kufika uchumi wa viwanda  pamoja na uchumi wa kati. https://youtu.be/_iefaEp1a8A

SIMU.TV: Jumla ya wanawake 30 wajasiriamali wa kata ya makumbusho jijini Dar es Salaam wamekabidhiwa taa zinazotumia nishati ya mwanga wa jua ili kuwarahisishia majukumu kwenye biashara zao nyakati za usiku. https://youtu.be/5dQhhpC2K6A

SIMU.TV: Ofisi ya taifa ya takwimu imesema mfumuko wa bei kwa mwezi February mwaka huu umeongezeka hadi kufikia asilimia 5.5 kutoka asilimia 5.2 ya mwezi January. https://youtu.be/Ujew_lHYRGo

SIMU.TV: Timu tatu za wanawake za mpira wa pete kutoka Tanzania zinatarajiwa kushiriki michuano ya kusaka bingwa wa Afrika Mashariki jijini Nairobi yatakayoanza April 23 mwaka huu. https://youtu.be/OL4KkzoGMXc

SIMU.TV: Mashindano ya soka yaliyoandaliwa na chama cha mpira wa miguu wilaya ya Ubungo UFA yanatarajiwa kuanza March 11 mwaka huu. https://youtu.be/P1809b7ryMk
SIMU.TV: Timu ya taifa ya wanawaake ya Ufaransa imetwaa ubingwa wa michuano maalumu baada ya kuifunga Marekani kwa mabao matatu kwa sifuri jana usiku. https://youtu.be/Dy7c3HBswmA

SIMU.TV: Baadhi ya wakazi wilayani Ilemela mkoani Mwanza, hawana sehemu za kuishi baada ya nyumba zao kukumbwa na mafuriko; https://youtu.be/FPSznOXeCRQ

SIMU.TV: Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, amewataka wanaume na wanawake nchini kujenga tabia ya kuheshimiana na kushirikiana; https://youtu.be/SH7W78n-hqs

SIMU.TV: Mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyavtva, ametoa wito kwa wanawake nchini kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za maamuzi katika jamii; https://youtu.be/X3YSyspt29g

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja Idrisa Hua, amesema ukosefu wa ujuzi wa uzalishaji bidhaa na masoko ni baadhi ya changamoto zinazokwamisha maendeleo ya mwanamke; https://youtu.be/X_WovzG3NVk

SIMU.TV: Waziri wa Elimu Prof Ndalichako, amesema Tanzania ni nchi mojawapo barani Afrika inayotambua mchango wa mwanamke katika ujenzi wa uchumi; https://youtu.be/w2SMARAWGcg

SIMU.TV: Baadhi ya wakazi katika eneo la Jangwani jijini Dar Es salaam wamekumbwa na taharuki baada ya Mafuriko kuvamia eneo hilo; https://youtu.be/NvVLTxWeNg0

SIMU.TV: Mfumuko wa bei kwa mwezi February mwaka huu umezidi kupanda mpaka kufikia asilimia 5.5 ukilinganisha asilimia 5.2 kwa mwezi uliopita; https://youtu.be/sXEtSQTQHXk  

SIMU.TV: Taasisi ya ujasiriamali na ushindani inawataka vijana kuchangamkia fursa za mafunzo ya ujasiriamali ili kujikwamua kiuchumi; https://youtu.be/_mcSUjtDwX4
SIMU.TV: Kampuni ya mafuta ya Total kwa kushirikiana na kampuni ya Intergrated Communication wametoa taa za Solar kwa wanawake wajasiriamali eneo la Mwananyamala; https://youtu.be/tFANPh-9ujI  

SIMU.TV: Chama cha Netiboli nchini kimesherehekea siku ya wanawake duniani kwa kuzikutanisha timu za Jeshi Star na Makongo katika dimba la Uhuru jijini Dar ; https://youtu.be/7PRIIDEQzCs

SIMU.TV: Kifimbo cha Malkia kinatarajia kuwasili nchini April 8 kama ishara ya kuanza kwa michuano ya Olimpiki; https://youtu.be/DAHB1-q8LfY

SIMU.TV: Msanii wa muziki wa Injili Christina Shusho amewataka wanawake kujituma na kujithamini katika kazi ili waweze kutambuliwa katika jamii; https://youtu.be/j-AL9NZBPHs



No comments: