Thursday, March 9, 2017

MWANAMITINDO KHADIJA MWANAMBOKA AADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUJUMUIKA NA MARAFIKI

Wakati Tanzania na Dunia nzima kwa ujumla zikiadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, leo Machi 8, 2017, Mwanamitindo nguli hapa nchini na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Vitu Vya Khadija, Bi Khadija Mwanamboka aliungana na wanawake wengine jijini Dar es salaam katika kuisherehekea siku hiyo muhimu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwanamboka alisema kuwa aliamua kuwaalika marafiki zake katika siku hiyo ili kuwataarifu mpango wake mpya alioupata kupitia Shirika lisilo la kiserikali la Sense International la nchini Uingereza lenye nia ya kuwasaidia watoto wenye ulemamu wa kusikia na kuona kwa pamoja waliopo hapa nchini, ambapo wataanzisha kitu kinaitwa Pendeza Kids Collection kwa kubuni mavazi mbalimbali ambayo yatauzwa katika Duka la Shirika hilo la Sense lililopo nchini Uingereza na zingine zitauwa hapa hapa nchini ili kuwasaidia watoto hao.

Hafla ya kuisherehekea siku hiyo adhimu kwa kina mama, ilifanyika katika Ukumbi wa Kamarambezi, Seacliff jijini Dar es salaam.
Khadija Mwanamboka (kati) akiwa na Marafiki zake waliofika kumuunga mkono katika mpango wake mpya wa kuwasaidia Watoto wenye ulemavu wa kusikia na kuona alioshirikiana na Kam
Sehemu ya Marafiki wa Khadija Mwanamboka waliohudhulia hafla hiyo.
































No comments: