Meneja wa Shirika la kuhudumia viwanda vidogovidogo Sido Mkoani Pwani Agnes Yesaya wa kushoto akiwa na Mwenyekiti wa kikundi cha Tuwenao wa kulia Sophia Mwaya mara baada ya kumkabishi cheki ya kiasi cha shilingi milioni mbili kwa ajii ya kikundi.
NA VICTOR MASANGU , MKURANGA
SHIRIKA la kuhudumia viwanda vidogovidogo (SIDO) Mkoa wa Pwani katika kuunga kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kupambana na wimbi la umasikini limevisaidia kuvikopesha vikundi viwili vya ujasiriamali kiasi cha shilingi milioni tatu kwa ajili ya kuweza kuwasaidia kuendeshea katika shughuli zao za kilimo kwa kuweza kuzalisha na kusindika wenyewe zao la muhogo .
Akizungumza na baadhi ya viongozi na wajumbe wa vikundi hivyo vya ujasiriamali vya Tuwenao pamoja Mponga vilivyopo Wilayani Mkuranga katika halfa fupi ya kukabidhi cheki ya fedha iliyofanyika katika kiwanda kidogo cha kusindikia muhogo Meneja wa SIDO Mkoa wa Pwani Agness Yesaya amesema kuwa wameamuakuvisaidia vikundi vya wajasiliamari wadogo waliopo vijijini kwa lengo la kuweza kuwawezesha ili kuwainua kiuchumi na kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo.
Baadhi ya viongozi wa Sido wakiwa wanatoka katika kiwanda kidogo cha kusindika zao la muhogo kilichopo katika kijiji cha Mpongo Wilayani Mkuranga.
Meneja Yesaya alisema kwamba wamebaini katika maeneo mengi ya vijiji kuna fursa nyingi zilizopo katika zao la muhogo lakini wamebaini kuwepo kwa baadhi ya wajasiriamali wanshindwa kutimiza malengo yao waliyojiwekea kutokana na kukosa mtaji wa fedha hivyo wakiwezeshwa wataweza kutumia fursa zilizopo za kilomo kwenye maeneo yao ili kuleta mabadiliko chanya ya kukuza uchumi.
Aidha Meneja huyo aliongeza kuwa Shirika hilo lengo lake kubwa ni kuwasaidia fedha za mitaji wajasiriamali wadogo wadogo waweze kujiendeleza zaidi ikiwemo sambmba na kuwajengea uwezo wa kuweza kusindika mazao yao katika ubora unaotakiwa kwa kuweka bidhaa zao katika vifungashio maalumu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kikundi cha ujasiliamari cha Tuwenao kilichopo katika kijiji cha Visegese Sophia Mwaya amelipongeza shirika la Sido kwa kuwapatia mkopo huo licha ya kukabiliwa na changamoto ya sugu ya kuharibiwa mazao yao mashambani na wanyama pori ikiwemo na ugonjwa wa bato bato hivyo kuiomba serikali kuliingilia kati suala hilo kwani linawarudisha nyuma kimaendeleo na kujikuta wanakosa chakula.
Mwenyekiti huyo alisema kwamba wana imani endapo vikundi vidogo vidogo vya wajasiriamali ambavyo vipo katika maeneo ya vijijini vikiwezeshwa kwa kupatiwa fedha vitaweza kuleta mabadiliko makubwa ya kuleta maendeleo kupitia mazao ambayo wanayalima hivyo ni vema serikali ikajikita zaidi katika kuwapa sapoti ya hali na mali ili waweze kutimiza malengo yao.
“Sisi kama kikundi nia yetu ni kuweza kufika mbali na kiukweli tnashikuru sana uongozi mzima wa Shirika la Sido Mkoa wa Pwani chini ya Meneja wake Agness Yesaya ameweza kututembelea mara kwa mara na kutuwezesha kiasi cha fedha ambazo kwa kweli tutazitumia vizuri katika kufanya yale yote ambayo tumeelekezwa,” alisema Sophia.
Nao baadhi ya wakulima wadogo wadogo wa zao za muhogo katika kijiji cha Mponga kilichopo Wilayani Mkuranga akiwemo Ramadhani Lusambi na Rehema Ngulangwa wamesema kwa sasa bado wapo katika hali ya sintofahamu kutokana na mazao yao kuliwa na wanyama sambamaba na kukabiliwa na tatizo kutokuwa na vifungashio kwa ajili ya bidhaa zao.
SHIRIKA hilo la kuhudumia viwanda vidogovidogo (SIDO) Mkoa wa Pwani limeamua kujikita zaidi kuvisaidia vikundi cha ujasiriamali vilivyopo katika maeneo ya vijijini kwa lengo la kuweza KUANZISHA vidogo na kuwakopesha fedha wananchi kwa ajili ya kuweza kuendeshea shughuli zao mbali mbali za kilimo ili kuweza kijikwamua kiuchumi na kuondoka na umasikini.
No comments:
Post a Comment