Friday, March 24, 2017

SERIKALI YASISITIZWA KUONGEZA MASUALA YA MABADILIKO YA TABIANCHI KATIKA MIPANGO NA BAJETI

Mkurugenzi Mtendaji wa ForumCC, Rebecca Muna akiwasilisha mada kwa wadau kutoka kwenye asasi za kiraia, maafisa mipango wa wizara mbalimbali pamoja na watafiti kuhusu namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti.

FORUMCC imeandaa mkutano na kukutanisha wadau kujadili namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti ya serikali kuu na serikali za mitaa hapa nchini Tanzania. 

Mkutano huo umewakutanisha wadau mbalimbali kutoka sekta binafsi pamoja na serikali ili kuangalia njia nzuri zinazoweza kusadia Tanzania kuwa na mfuko wa Mabadiliko ya Tabianchi ili kupunguza kutegemea zaidi fedha kutoka kwa wafadhili.

Lengo la mkutano huu ni kuwakutanisha wadau kujadili na kuhamasisha jitihada za kuingiza masuala ya mabadiko ya Tabianchi katika mipango na bajeti ya Serikali katika kipindi hiki tunapoelekea katika Bunge la bajeti ya mwaka 2017/18.

Akizungumza kwenye mkutano huo Mkurugenzi Msaidizi, Sekta za Uchumi na Uzalishaji toka TAMISEMI, Dkt. Lucy Ssendi amesema serikali kupitia TAMISEMI iko karibu na wadau mbalimbali wa mabadiliko ya Tabianchi ili kuweza kupunguza majanga mbalimbali hapa nchini, na wao TAMISEMI wana jukumu la kubwa kwenye asasi za kiraia kuingia kwenye miradi inayohusu mabadiliko ya Tabianchi.

Pia Mwenyekiti wa bodi ya ForumCC, Euster Kibona aliwaomba wadau mbalimbali waliofika kwenye mkutano huo kushirikiana na FORUMCC ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea kwenye suala la mabadiliko ya Tabianchi linalotishia maendeleo ya jamii za mbalimbali na ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.

Mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa COSTECH (Tume ya Sayansi na Teknolojia) leo uliwakutanisha wadau mbalimbali kutoka asasi za kiraia, maafisa mipango kutoka wizara mbalimbali, watafiti na waandishi wa habari. 
Mkurugenzi Msaidizi, Sekta za Uchumi na Uzalishaji toka TAMISEMI, Dkt. Lucy Ssendi akitoa mada kuhusu kazi za TAMISEMI pamoja na ushirikiano wake kwenye masuala ya mabadiliko ya Tabianchi kwenye mkutano uliofanyika leo kwenye kumbi wa COSTECH (Tume ya Sayansi na Teknolojia) jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa bodi ya ForumCC, Euster Kibona akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali pamoja na kutoa maoni kwa maofisa wa wizara kuangalia namna ya kushirikiana ili kupunguza athari za mabadiliko ya Tabianchi.
Mkutano ukiendelea uliowakutanisha wadau mbalimbali uliowakutanisha ili kujadili namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti.
Mtaalamu wa Masuala ya Nishati, Erneus Kaijage akiwasilisha mada kuhusu uwekezaji wa fedha katika sekta ya nishati kwenye mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa mabadiliko ya Tabianchi leo jijini Dar es Salaam






Baadhi ya wadau wa Mabadiliko ya Tabianchi wakichangia mada pamoja na kuuliza maswali kuhusu namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa COSTECH (Tume ya Sayansi na Teknolojia) leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Msaidizi, Sekta za Uchumi na Uzalishaji toka TAMISEMI, Dkt. Lucy Ssendi akijibu maswali yaliyokuwa yanaulizwa na wadau mbalimbali wa masuala ya mabadiliko ya Tabianchi kwenye mkutano uliowakutanisha wadau hao kwenye ukumbi wa Chuo cha Sayansi jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa ForumCC, Rebecca Muna akijibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wadau mbalimbali waliokutana ili kujadili namna ya kuongeza jitihada katika kuingiza masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi katika mipango na bajeti.
Mwezeshaji wa Mkutano wa FORUMCC, Abdallah Henku akizungumza jambo kwenye mkutano huo uliowakutanisha wadau mbalimbali wa Mabadiliko ya Tabianchi.



Baadhi ya wadau mbalimbali walioshiriki kutoka asasi za kiraia, maafisa mipango kutoka wizara, watafiti na waandishi wa habari wakifuatilia mada zilizokuwa zikiendelea kwenye ukumbi wa COSTECH (Tume ya Sayansi na Teknolojia) mkutano ulipofanyika leo ulioandaliwa na FORUMCC.

Picha ya Pamoja

No comments: