Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri wa miaka 17 maarufu kwa
jina la Serengeti Boys jana Jamatano wamefanya mazoezi kujiweka tayari na mchezo wao wa kesho na Timu ya U17 ya Burundi.
Serengeti Boys
itakuwa kambini Bukoba hadi Aprili 2, mwaka huu ambako inatarajiwa
kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu vijana ya
Burundi kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani hapa Kagera. Michezo
hiyo itaanza kuchezwa Machi 30, 2017 na kurudiana Aprili mosi, mwaka huu.
Serengeti
Boys ambayo inajiandaa na michuano Afrika huko Gabon itarejea Dar es
Salaam Aprili 2, mwaka huu ambako imepangwa kucheza na Ghana Aprili 3,
mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo utatanguliwa
na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.
Timu itaelekea
Morocco Mei 5, mwaka huu baadaye itapita Cameroon kwenye kambi ya zaidi
ya mwezi mmoja baadaye itakwenda Gabon katika michuano itakayoanza Mei
14, 2017. Ikiwa Cameroon itacheza mechi mbili za kimataifa dhidi ya
wenyeji kabla ya kwenda kwenye fainali.
Serengeti Boys ni timu
ya vijana ambayo imefuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika
zitakazofanyika Gabon kuanzia Mei 14, mwaka huu. Timu hiyo imepangwa
Kundi ‘B’ pamoja na mabingwa watetezi Mali, Niger na Angola. Ina lengo
la kurejea na Kombe la Afrika kwa vijana.
Na ikitokea imekosa
nafasi hiyo angalau ikafika nusu fainali ambako kwa mafanikio hayo
itakuwa tayari ina tiketi mkononi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia
huko India, Novemba, mwaka huu.
Kikosi cha Serengeti Boys kinaundwa na Makipa: Ramadhan Kabwili, Samwel Edward na Kelvin Kayego.
Walinzi: Kibwana Ally Shomari, Nickson Kibabage, Israel Mwenda, Dickson Job, Ally Msengi, Issa Makamba na Enrick Vitalis Nkosi.
Viungo:
Kelvin Nashon Naftali, Ally Ng’anzi, Mohamed Rashid, Shaaban Ada,
Mathias Juan, Marco Gerald, Abdulhamis Suleiman, Saidi Mussa na Cyprian
Benedictor Mtesigwa.
Washambuliaji: Muhsin Malima Makame, Yohana Mkomola, Ibrahim Abdallah, Assad Juma na Abdul Suleiman.
Benchi la Ufundi:
Bakari Shime (Kocha Mkuu)
Oscar Mirambo (Kocha Msaidizi)
Muharami Mohamed (Kocha wa makipa)
Kim Poulsen (Mshauri wa Ufundi)
Edward Evans (Mtunza Vifaa)
Shecky Mngazija (Daktari wa timu)
Serengeti Boys watacheza mchezo wao wa kwanza kesho jioni na Timu ya U17 ya Burundi ambayo imeingia Bukoba hii leo jioni kwenye muda wa saa 11 na hatimaye hawakuweza kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa Kaitaba kutokana na uchovu wa safari yao na hivyo kutoa taarifa kuwa watafanya asubuhi saa moja.
No comments:
Post a Comment