Thursday, March 30, 2017

MAKAMU WA RAIS WA KLABU YA SIMBA, GEOFREY NYANGE KABURU AZINDUA TAWI LA SIMBA LA KICHWABUTA LEO BUKOBA

Makamu wa Rais wa Klabu ya  Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburu jana amefungua Tawi la kwanza la  Simba mjini Bukoba na kuweza kuwaunganisha Wana Simba wa hapa Kagera. Pia katika Uzinduzi huo wa Tawi ambalo lipo Kashabo pia walikuwepo Wachezaji wa Simba wakiongozwa na nahodha Jonas Gerald Mkude, Kichuya na Wengine. Piacha na Faustine Ruta, Bukoba
Pia wameweza kumshukuru ndugu Omary Makoye, Mratibu wa Tawi wa Klabu ya Simba kwa kuwatembelea wakiwa katika Mchakato wa kuunda Tawi hilo. Na pia wameshukuru kwa msaada aliowapa na ulikuwa ukihitajika kwa muda huo. Shukrani pia kwa Ndugu Sued Mkwambi kwa kukubali kuwa mlezi wao wa Tawi.
Makamu wa Rais wa Klabu ya  Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburuakiteta na Wanatawi na wanakagera waliokuwa eneo la Tawi hilo la Kichwabuta.

Mh. Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburu(wa pili) kutoka kushoto akiwa na  Viongozi wa Tawi la Kichwabuta lililozinduliwa leo hii mjini Bukoba. Tawi hilo limepewa Jina la Kichwabuta kutokana na kuenzi kazi ya Mwananchama maarufu wa Klabu ya Simba MZEE HUSSEIN OMARY KICHWABUTA ambaye alishiriki kikamilifu kama mpenzi na Mwanachama wa Simba katika maendeleo ya Klabu hiyo ya Simba. Tawi hilo mpaka sasa lina Wanachama 160 waliojiandikisha na taratibu zinaendelea kuhakikisha wanapata kadi za uanachama kulingana na utaratibu wa Klabu. Tawi linaongozwa na Mwenyekiti Ndugu Priscus Isdory Massawe, Katibu ndg. Fauzu BinaMungu, Mhasibu Ndg. Dickson Ishengoma, Msemaji Ndg. Miraji Kichwabuta na Viongozi wengine ili kuhakikisha wanapata Wanachama wengi zaidi.
Wadau na Wapenzi wa Simba wakiwa tayari kwa Uzinduzi wa Tawi hilo.Wakifuatilia kwa karibu Uzinduzi wa TawiMakamu wa Rais wa Klabu ya  Simba, Ndg. Geofrey Nyange Kaburu akisaini kwenye Kitabu 

No comments: