Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli ametoa wito
kwa Watanzania kuulinda mradi wa barabara za juu kwenye makutano ya
barabara za Morogoro,Mandela na Sam Nujoma eneo la Ubungo Jijini Dar es
Salaam utakaogharimu shilingi bilioni 188 na kukamilika mwaka 2019.
Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akitoa hotuba kabla ya kuweka jiwe la msingi la barabara za juu eneo la Ubungo.
“Tutasimamia
pesa izi kikamilifu ili tujenge barabara izi za juu vyema,nawataka
Watanzania kusimamia mradi huu ili ukamilike haraka na hivyo
Wizara,Mkandarasi na Msimamizi wa mradi ili ulete ukamilike na kuleta
tija kwa wananchi hawa”,Aliongeza Rais Magufuli.
Amesema
katika ujenzi wa mradi huo bilioni 1.9 inatoka Serikalini na bilioni
186 inatoka Benki ya Dunia na ivyo ni muhimu kuulinda kwani ni pesa za
Watanzania walipa kodi.
Aidha amesisitiza kuwa nchi ya yetu imepata mkopo huu kwa sababu tunaaminika katika kukopesheka na tunarudisha kwa wakati,amemuomba rais wa benki ya Dunia kuendelea kuikopesha Tanzania katika miradi mingine.
Rais
Magufuli ameeleza kuwa mkopo huu kutoka benki ya Dunia una riba ya
asilimia 0.5 na unalipwa ndani ya miaka 40 ivyo ni vyema kuendelea
kushirikiana na Benki ya Dunia.
Pamoja
na hayo amewataka Watanzania kuendelea kulipa kodi itakayowezesha ili
Serikali iendelee kutekeleza miradi mingine na kuongeza kuwa kukamilika
kwa mradi huu kutatoa sura ya pekee ya jiji la Dar es Salaam na
kupunguza msogamano wa magari kwa kiasi kikubwa sana.
Kwa
Upande wake Rais wa Benki ya Dunia Dkt.Jim Yong Kim ametoa shukurani
kwa Serikali ya Tanzania na kusema kuwa ameshawishika kuja nchini baada
ya kusikia vongozi wengi wa Dunia wakisifia jitihada za Rais Magufuli za
kuunda upya Serikali yake ikiwa ni pamoja na kupunguza matumizi na
kuwekeza katika kujenga miundombinu na elimu.
“Tanzania
inaelekea kuwa Taifa la watu wa kipato cha kati miaka nane ijayo na
kila mtu kuwa na bima ya afya,elimu bora na muono mzuri wa mbeleni,na
njia pekee ya kufika huko ni kujitegemea na kutumia rasilimali za
nyumbani katika mkakati bora kabisa na hivyo kupunguza kabisa misaada ya
nje ambayo imeshuka hapa nchini kwenu,”Aliongeza Dkt.Jim Yong Kim
Aidha
amesema kuwa tangu kufunguliwa kwa Mabasi ya Mwendo kasi imepunguza
msongamano kwa dakika 90 kwa siku na hivyo ufunguzi wa biashara mpya pia
umeenda sambamba.
Amesisitiza kuwa Benki ya Dunia itaendelea kusimama pamoja na Tanzania katika maendeleo na kufanya kazi pamoja.
No comments:
Post a Comment