Thursday, March 16, 2017

Jesca Honole maarufu kama ‘Jesca BM.’achomoza tamasha la pasaka

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo mchana jiini Dar kuhusiana na maandalizi ya tamasha la Pasaka ambalo linatarajiwa kufanyika Aprili 16 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa likishirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akifafanua jambo jambo kwa kina mbele ya waandishi wa Habari (hawapo pichani) jijini Dar leo kuhusu maandalizi ya tamasha la Pasaka ambalo linatarajiwa kufanyika Aprili 16 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa likishirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili.


KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka chini ya mwenyekiti wake Alex Msama, limeanza kutaja waimbaji wa nyimbo za injili watakaoshambulia ‘tamasha la mwaka huu.

Mwimbaji wa kwanza kutajwa na Kamati hiyo katika mkutano wake na waandishi habari jijinin Dar es Salaam leo , ni Jesca Honole maarufu kama ‘Jesca BM.’

Msama amesema leo kwamba, mwimbaji huyo amepata bahati ya kipekee ya kuwa wa kwanza na kwamba wengine watawekwa hadharani baada ya kupitishwa rasmi na Kamati.

“Tunamshukuru Mungu kwa sababu maandalizi ya Tamasha letu la Pasaka ambalo safari hii linakuja kitofauti zaidi, waimbaji wameanza kupitishwa, ikiwa ni hatua nzuri ya tukio hili la kimataifa,” alisema Msama na kuongeza.

‘Mwimbaji aliyebahatika kuwa wa kwanza kuthibitishwa ni Jesca Honoli maarufu kama ‘Jesca BM’, mmoja wa waimbaji mahiri kwa sasa.

Alisema nguvu ya kuanza kutangaza waimbaji watakaohudumu katika Tamasha hilo litakaloanzia Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam April 16, ni baada ya kupata kibali rasmi cha tukio hilo.

Kuhusu kibali, Msama ametoa shukrani kwa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa kutoa baraka kwa tukio hilo la kimataifa ambalo litatikisa katika mikoa ipatayo mitano ya Tanzania bara.

Alisema, baada ya Tamasha hilo kuzindiliwa April 16 katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, litahamia Uwanja wa Jamhuri, mjini Dodoma kabla ya kutua katika mikoa mingine mitatu.

Alisema mbali ya Tamasha hilo kubeba malengo yake ya msingi yakiwamo ya kueneza neno la Mungu na kutumia sehemu ya mapato kufariji makundi maalumu, safari hii litatumika kama jukwaa la kumuombea nch Rais John Pombe Magufuli na nchi kwa ujumla.

Manufaa mengine ya Tamasha hilo linalofanyika tangu mwaka 2000, ni kuweza kukuza muziki wa injili kiasi cha kuwa ajira kwa vijana wenye vipaji.

No comments: