Tuesday, March 28, 2017

BoT YAWAPIGA MSASA WAANDISHI WA HABARI ZA UCHUMI NA FEDHA


Mchumi Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, Bw. Lusajo Mwankemwa, akiwasilisha mada juu ya Sera ya Fedha ya Benki Kuu ya Tanzania, wakati wa semina ya Wiki moja kwa waandishi wa habari za Uchumi na Fedha kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, tawi la Zanzibar, leo Machi 28, 2017.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said


MFUMUKO wa bei utokanao na ongezeko la Fedha ni hatari sana katika uchumi wa nchi, Mchumi Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, Bw. Lusajo Mwankemwa, ameiambia semina ya Waandishi wa habari za Uchumi na Fedha kutoka vyombo mbalimbali vya habari leo Machi 28, 2017.

Semina hiyo ya wiki moja inayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania tawi la Zanzibar, ina lengo la kuwaelimisha waandishi wa habari kuhusu namna bora ya uandishi w ahabari za uchumi na fedha.

Chini ya Sera ya Fedha, (Monetary Policy), Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), kama mtengeneza fedha (mchapishaji), inaweza kudhibiti mfumuko wa bei utokanao na ujazi wa fedha kutokana na viashiria vya uwezo wa uzalishaji katika taifa unapopungua au kuonegzeka. Sera ya fedha maana yake ni pale Benki Kuu inapoamua kuongeza fedha kwenye mzunguko au kupunguza na hii itategemea sana na uzalishaji bidhaa, alifafanua Lusajo.

“Inapogundulika kuwa kiwango cha fedha ni kikubwa kwenye mzunguko kuliko uzalishaji BoT kazi yake hapa ni kupunguza fedha kwenye mzunguko na hii sio kwa eneo fulani tu la nchi bali ni nchi nzima ambako fedha ya Tanzania inatumika.” Alisema Mchumi huyo.

Akifafanua zaidi kuhusu namna BoT inavyoshughulikia ujazi wa fedha au kupunguza, Lusajo alisema njia pkee inayotumika ni kupitia mabenki ya biashara.

“Kama mjuavyo bei ya Mafuta inadhibitiwa na soko la Dunia, na hata mfumuko wa bei za vyakula unategemea na tabia nchi kama ukame unaopelekea upungufu wa chakula, hapa BoT inachofanya ni kutoa usahuri kwa Serikali ili kupitia vyombo vyake ikiwemo vile vya kodi kufanyia kazi hali hiyo.” Alifafanua Mchumi huyo Mwandamizi wa BoT.

Alisema moja ya hatua za kuongeza ujazi wa fedha kwenye mzunguko ni hatua ya hivi karibuni ya Benki Kuu, (BoT), kupunguza kiwango cha amana zinazowekwa na mabenki ya biashara kwenye Benki Kuu, kutoka asilimia 10 hadi asilimia 8.

“Hii ina maana asilimia 2 ambayo Benki Kuu imeondoa, sasa mabenki ya biashara yanaweza kukopesha wananchi na hivyo ujazo wa fedha kuongezeka kwenye mzunguko.” Alisema Lusajo.

Ieleweke kuwa fedha ili ziongezeke kwenye uchumi lazima zipitie kwenye mabenki ya biashara ambayo yatazitoa kwa wananchi kupitia mikopo. “Na mikopo itolewayo na mabenki iko mingi sana na kwenye taasisi nyingi kama vile SACCOS, VICOBA na hata wafanyabiashara mbalimbali wakiwemo wakubwa na wadogo na watu binafsi pia, alisema

Mchmi huyo pia alisema, Watanzania wengi hawana utamaduni wa kuweka fedha benki ili kuziwezesha benki hizo nazo kuwa na uwezo wa kuwakopesha zaidi wananchi.

Hata hivyo kiwango cha fedha kinachotolewe na mabenki ya biashara hapa nchini ni kidogo kuliko kile ambacho watu wanataka kukopa na hivyo ili mabenki hayo yaweze kukopesha, lazima benki hizo nazo zikope kwa mabenki mengine yawe ya ndani au nje ya nchi.

“Hivyo benki za biashara kwa vile inapaswa kulipa riba huko ilikokopa, na kulipa mishahara wafanyakazi wake, mtu atakayewkenda kukopa lazima alipe riba ya asilimia 20 kwa mfano na ukimuuliza kwanini unamtoza riba hii ya asilimia 20, atakwambia, mimi nimekopa ili niweze kuwakopesha watanzania ambao wengi hawapendi kuweka fedha benki, alifafanua

Akifafanua zaidi, Mchumi huyo alisema, hivi karibuni BoT, imepunguza riba kutoka asilimia 16 hadi asilimia 12 kwa benki za biashara zinazokwenda kukopa Benki Kuu ili ziweze kutoa mikopo kwa wananchi. Alifafanua Lisajo
Meneja Uhusiano wa Umma na Itifaki wa Benki Kuu ya Tanzania, BoT), Bi. Zalia Mbeo, akifafanua baadhi ya hoja zilizoulizwa na waandishi wa habari kuhusu mada ya Sera ya Fedha.

Baadhi wa Waandishi wa habari wakifuatilia mada hiyo
Meneja Msaidizi-Idara ya Uhusiano wa Umma, Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bi. Vicky Msina akizunhuzma mwanzoni mwa warsha hiyo.
Mwandishi wa habari za Biashara na Uchumi wa Azam TV, Bi. Rahma Salum akizungumza



Bw.Genes Kimari, (kushoto), na Bw. Mohammed Kailwa wote kutoka Kurugenzi ya Masoko ya Fedha -BoT 
Meneja Masoko ya Ndani Kurugenzi ya Masoko ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bw.Reverian Mbeo, akizunhuzma wakati akiwasilisha mada juu ya Majukumu ya Kurugenzi ya Masoko ya Fedha, Utekelezaji wa sera ya fedha wa Benki
Kutoka kulia, Meneja wa Fedha na Utawala, Bodi ya Bima ya Amana ya BoT, Bw. Richard Malisa, Meneja Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Bi. Zalia Mbeo, Mchumi Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, BoT, Bw. Lusajo Mwankemwa, na Bw.Mohammed Kailwa kutoka Kurugenzi ya Masoko ya Fedha, BoT.

No comments: