Sunday, February 26, 2017

WALIOBOMOLEWA NYUMBA ZAO WAMWAGUKIA MBUNGE WA JIMBO LA GEITA MJINI.

Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini ,Constatine Kanyasu,akizungumza na wananchi wa kata ya Buhala hala wakati aliipokwenda kusikiliza kero ambazo zimekuwa zikiwakabili kwenye maeneo ambayo wanaishi.
Maeneo ambayo wananchi walibomolewa nyumba zao.
Moja kati ya wananchi ambao wameuzulia Mkutano huo akielezea kero yake kwa Mbunge wa Geita mjini wakati wa Mkutano huo.
Meza kuu ikiongozwa na Mbunge wa Geita,Mjini,Diwani wa kata ya Buhala hala pamoja na baadhi ya wajumbe wakifatilia maelezo kutoka kwa wananchi.
Wananchi ambao walikuwa wamejitokeza kwenye mkutano huo wakisikiliza wakati Diwani wa kata ya Buhala hala alipokuwa akitoa maelezo na kujibu baadhi ya changamoto za wananchi.
Steven John ambaye ni moja kati ya wananchi ambao wamebomolewa makazi yao akielezea namna ambavyo alivyo bomolewa makazi yake.
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Geita,ambaye pia ni afisa Mipango Luciano Bundala,akijibu kero za wananchi wakati wa mkutano wa mbunge wa Geita Mjini.
Diwani wa kata ya Buhala hala,Mussa Kabesse akifafanua na kutoa majibu juu ya maswali ambayo yalikuwa yameulizwa na wananchi.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE

Mbunge wa Geita Mjini Constatine Kanyasu amesikitishwa kwa kitendo cha wananchi waliokuwa wamejenga kwenye hifadhi ya misitu kubomolewa huku wengine wakiachwa katika maeneo hayo na kuahidi kushughulikia ili haki itendeke sawa na wale ambao hawajabomolewa.

Hayo aliyasema kwenye mkutano wa hadhara ambao umefanyika kwenye mtaa wa Mwatulole kata ya buhala hala wilaya na Mkoa wa Geita,wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika jimbo ambalo analiongoza.

Mh Kanyasu amesema kuwa amesikitishwa na hatua ya TFS kubomoa nyumba za watu wengine huku wale wenye uwezo wakiachwa na kuendelea kukaa kwenye maeneo hayo kutokana na hilo wameagiza watu wa TFS kuangalia kama wale waliobomolewa pale yalikuwa ni maeneo yao na ninani ambaye aliwauzia.

“Naomba Nikiri na mimi iliniuma sana lakini kwa sababu ni serikali na sikuwepo na sijui kama walitumia sheria mimi naomba yeyote ambaye ni haki yake ya msingi alete na mimi nitashughulikia”Alisema Kanyasu

Hata hivyo Bi,Chausiku Lusetula ambaye ni miongoni mwa wanananchi waliobomolewa makazi yao amemuomba Mbunge kuwasaidia ili wapate haki zao za msingi na kwamba kwa sasa hawana makazi ya kuishi baada ya makazi yao kubomolewa.

“Mheshimiwa Mbunge sisi ni watu ambao tumekosa makazi kwa sasa hatujui ni wapi tutaishi na chakusikitisha kwanini sisi tubomolewe na wengine waendelee kukaa kwenye maeneo ambayo inasemekana ni hifadhi ya misitu kama ni hivyo ni vyema haki itendeke kwa wote”Alisema Chausiku

Diwani wa kata ya Buhala hala ,Mussa Kabese amewaambia wananchi kuwa mbunge wa jimbo la Geita Mjini tayari amekwisha mwandikia Waziri mwenye dhamana barua ambayo imemwomba matumizi ya pori la buhala hala kubadilishwa na kuwekwa taasisi ambazo zitawasaidia wananchi ambao wapo kwenye mitaa ya shinde na magogo kupata mahitaji ya msingi ikiwemo swala la elimu na afya.

Hatua hii imekuja ni baada ya takribani wiki mbili kumalizika ambapo wananchi ambao wamejenga kwenye hifadhi ya misitu inayosimamiwa na wakala wa misitu nchini TFS kubomolewa makazi yao.

No comments: