Wafanyakazi wa Serikalini Wilayani Handeni wametakiwa kutoa
ushirikiano kwa namna yoyote ile kama kuna eneo wanatakiwa kutoa ushahidi
Mahakamani. Wametakiwa kuhudhuria mahakamani ili waweze kusaidia haki iweze
kupatikana kwa wakati.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin
Gondwe alipokuwa akihutubia wananchi na wataalamu mbalimbali kwenye ukumbi wa
Mahakama ya Wilaya ya Handeni jana katika maadhimisho ya siku ya sheria Nchini iliyoandaliwa na Mahakama ya Wilaya mwaka
2017 yenye kauli mbiu ya “ umuhimu wa utoaji haki kwa wakati kuwezesha
ukuaji wa uchumi”.
Gondwe alisema “amani na utulivu ndio matunda ya Haki,
sehemu yeyote iliyokosa amani na utulivu basi lazima kuna haki imepokonywa”
Kuli mbiu yetu inatukumbusha wadau wote ambao tunasimamia sheria kuanzia jamii
ya kawaida , wataalamu, mawakili, wanasheria ,TAKUKURU, uhamiaji na magereza
tuweze kufanya kazi kwa pamoja ili haki iweze kutendeka kwa wakati na kukuza
uchumi wetu.
Aidha alieleza kuwa TAKUKURU, Magereza, Uhamiaji , Wanasheria na
Mawakili wa Serikali na kujitegemea hawataweza kufanikiwa katika kupambana na
Rushwa na kutoa haki kama Mahakama haitakuwa mdau mkuu katika hili. Alisema
kuwa kwa kuliona hilo Mahakama imetoa elimu kwa
wananchi wiki nzima juu ya umuhimu wa utoaji wa haki kwa wakati
kuwezesha ukuaji uchumi.
Mahakama yenyewe imefahamu nafasi ya kusimama na kuweza kushirikiana na
wadau wote ili kuhakikisha kwamba wananchi wanoishi Handeni wanapata haki mbali
na changamoto mbalimbali zinazoikumba Mahakama hasa ukosekanaji wa watoa
ushahidi hali inayopelekea kuchelewa kwa kesi na maranyingine kufungwa kwa
kukosa ushahidi uliojitosheleza. Mwananchi anapodai haki lazima afahamu kuwa
anao wajibu wa kufanya ili haki hiyo aweze kuipata, alisema Mh. Gondwe.
Aliongeza kuwa Serikali inafahamu mabaraza ya ardhi yanamatatizo,
kwa kuliona hilo wanasheria wa Halmashauri ya Mji Handeni wameanza kuelimisha viongozi wa mabaraza ya
ardhi namna bora ya kusimamia kesi na wameelezwa jinsi gani ambavyo wakienda kinyume mabaraza
hayo yanaweza kuvunjwa kwani zipo taasisi nyingine kama TAKUKURU ambazo wanaweza
kushughulikia wakiukaji wa kanuni za mabaraza ya ardhi kama watu wengine ambao
sio waadilifu katika mifumo ya kiserikali. Viongozi wa Serikali wasitumie
mifumo ya kiserikali kujihalalishia mapato yasiyo halali. Upande wa Halmashauri
ya Wilaya ya Handeni Mkurugenzi na wanasheria waeanza mikakati ya kutoa elimu kwa mabaraza ya ardhi.
Mh. Gondwe Alieleza kuwa nyaraka nyingi za serikali zinatengenezwa
bandia, alivitaka vyombo vinavyohusika na utoaji haki kuhakikisha wanahakiki
nyaraka/vielelezo kutoka malaka husika ili viweze kuwa halali kwa utoaji wa
haki.
Mwisho alizitaka taasisi za Serikali kufanya kazi na kuhakikisha
zinawezesha Mahakama kwenye kesi ili kusaidia kesi hizo ziweze kuisha kwa
wakati na kuokoa muda ambao wananchi wanapaswa kushiriki katika kukuza Uchumi
mbali na jiografia ngumu ya Wilaya ya Handeni.
Mh. Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya Bw.Anorld Kileo alieleza kuwa
Mahakama kama muhimili wa Serikali ndio chombo pekee kinachotoa Haki. Dhima ya maadhimisho haya inatutaka sisi kama watendaji wa
Mahakama tuliokabidhiwa mamlaka ya kutoa haki tuweze kutoa haki kwa wakati ili
kuwezesha jamii kuweza kuendelea na shughuli zao za Uchumi wa mtu binfsi na
Taifa kwa ujumla.
Maadhimisho ya siku ya sheria Nchini hufanyika kila mwaka wiki ya kwanza ya mwezi
wa pili. Maadhimisho hayo yalijumuisha wadau
mbalimbali kutoka Halmashauri ya Mji na Vijijini Handeni wakiwemo
Wanasheria, Mawakili, Idara ya Uhamiaji, Magereza, TAKUKURU na Polisi, yenye
kauli mbiu ya “Umuhimu wa utoaji haki kwa wakati
kuwezesha ukuaji uchumi”.
Alda Sadango
Afisa habari
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe akihutubia wananchi na viongozi mbalimbali kwenye maadhimisho hayo
Afisa upelelezi Bw. Paul Kimaro akitoa hotuba fupi wakati wa maadhimisho ya sheria
Mkuu wa Wilaya na wataalamu mbalimbali wakati wa wimbo wa Taifa.
Waendesha mashtaka wa Wilaya ya Handeni Bw.Joseph Hamisi na Nzagalila Kikwelele wakisikiliza hotuba wakati wa maadhimisho.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wikaya ya Handeni Bw. Noel Abel akisalimia wananchi.
Wanasheria
wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. Amani Mangesho wa kwanza
kushoto na Bw. Joseph Vungwa wakijitambulisha kwa wananchi wakati wa
maadhimisho
Mh. Hakimu mkazi mfawidhi wa Wilaya ya Handeni na Kilindi Bw.Anorld kileo akitoa hutuba fupi wakati wa maadhimisho.
Moja ya mwananchi akitoa hoja ya kupatiwa ufafanuzi.
No comments:
Post a Comment