Saturday, February 4, 2017

CCM YASOMBA WANACHAMA WAPYA 102 WAKIWEMO WA CUF,CHADEMA NA ACT WAZALENDO WILAYANI KAKONKO MKOANI KIGOMA


Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma imevuna jumla ya wanachama wapya 102 kutoka chama cha Act Wazalendo na Chama cha Wananchi Cuf.

Wanachama hao ambao wamepokelewa na mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma Prof Joyce Ndalichako ambaye aliwakabidhi wanachama hao wapya kadi 102 , akiwemo Mwenyekiti wa Chama cha ACT wazalendo Wilaya ya Kakonko pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF Wilayani humo .

Zoezi hilo alilifanya jana katika Sherehe za maadhimisho ya Miaka 40 ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kakonko, ambapo Wanachama kutoka katika Vyama vya ACT wazalendo, NSSR Mageuzi, CHADEMA na Chama cha Wananchi CUF ambao waliamua kuvihamba Vyama hivyo kutokana na Waanzilishi wa Vyama hivyo kukosa uzalendo kwa Nchi yao kwa kuwashawishi viongozi walio chaguliwa na vyama hivyo kuipinga Serikali katika masuala ya Maendeleo.

Sambamba na zoezi hilo Ndalichako aliwaomba Wanachama Wa CCM Wilayani humo katika uchaguzi wa viongozi wa Chama 2017 kuhakikisha Wanachagua viongozi wazalendo Wanaoweza kukijenga chama katika Misingi ya Uzalendo, amani na mshikamano kama Waanzilishi wa Chama hicho walivyo kijenga Chama hicho ambacho kinazidi kuwa ni Chama kinacho wajali wanyonge.

Alisema Kauli mbiu ya maadhimisho ya Miaka 40 ya Chama Cha mapinduzi ni CCM mpya na Tanzania mpya .kauli hiyo haiwezi kukamilika endapo chama hicho kitapata viongozi wasaliti wasio na mapenzi na Chama ambao wengi wao wametumika kununuliwa na vyama vya upinzani katika kipindi cha uchaguzi wa mwaka 2015 ambapo CCM imepoteza majimbo wengi kutokana na viongozi hao waliokisaliti Chama.

"Nianze kwa kuwapongeza Wanachama walio amua kurudi katika Chama cha Mapinduzi wamefanya jambo zuri sana, CCM ni chama ambacho kikitoa ahadi zake lazima zikamilike na ni chama chenye misingi ya uwajibikaji, uzalendo amani na ushirikiano ndio maana Wananchi wengi wanaendelea kukiamini chama chetu kutokana nuwaombe Wanachama Wenzangu tusikubali kurubuniwa na baadhi ya watu wasio kipenda chama kikiuka Misingi ya Waanzilishi Wa chama chetu walioiweka ambayo inatusaidia Chqma hiki kuwa na Amani na mshikamano tofauti na Vyama vingine", alisema Ndalichako.

Kwa upande wake Katibu Wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Wa Kigoma,Naomi Kapambala aliwashukuru Wanachama hao kwa kukiamini Chama hicho na kuamia kujiunga! Aliwaahidi Wanachama hao kuwa Chama hicho kitaendelea kutenda haki na kuwatumikia Wananchi katika misingi ya uwajibikaji na kujitegemea ilikuhakikisha Chama hicho kirudisha misingi yake ya zamani.

Hata hivyo Kapambala aliwaomba wanachama wote kuendelea kudumisha Umoja na mshikamano katika kuhakikisha Shughuli za chama hicho zinasonga mbele na Kwa kipindi cha uchaguzi wa mwaka 2017 wahakikishe Wanachagua viongozi Waadilifu,wasio penda rushwa na wanaotumiwa katika kukidhohofisha chama kutokana na maslahi ya baadhi ya Watu wasio penda Maendeleo ya Chama hicho.

Nao baadhi ya Wanachama walio hamia CCM, akiwemo Mwenyekiti wa ACT wazalendo Nikolaus Weslaus alisema ameamua kukihama chama hicho kutokana na Mapungufu yaliyomo katika Chama hicho, alisema kunamambo aliyo yagundu katika chama hicho ni kitu kimoja kinaanzia kwa viongozi wa Juu wavyama vya upinzani unaoleta msukumo Mkubwa kwa wanasiasa wake na wananchi ili Nchi hii isiweze kutawaliwa ikiwemo zoezi la kuwashawishi madiwani na Wabunge kupinga kila kitu kinachoendelea katika Serikali hata kama ni cha maendeleo bila sababu ya Msingi.

Alisema Ameamua kuhamia CCM kutokana na Rais aliyepo madarakani anasisitiza suala la uwajibikaji na vita dhidi ya rushwa ambavyo vimekuwa vikwazo vikubwa vya kuzuia maendeleo ya Nchi hii na Zoezi hilo linaendelea Kukamilika bila shida yoyote na serikali inaendelea kuwahudumia wananchi wote kwa usawa bila kuangalia chama.

Amana Ramadhani ni Mwenyekiti wa Chama cha wananchi CUF Wilaya ya Kakonko alisema ameingia kwenye chama hicho tangu mwaka 1997 kutokana na chama hicho kuwa na sera nzuri na kwakuwa na malengo mazuri ya kuisaidia Serikali katika kupata Suqla zima la Demokrasia pamoja na maendeleo, lakini mpaka sasa kitu alicho kitalajia katika Chama hicho hajakiona.

Na kilicho mfanya kuhamia CCM ni baada ya kuona Serikali ya Awamu ya Tano inavyo tekeleza Ilani yake kama ilivyo ahidi kipindi cha Kampeni na Sasa wanaendelea kuitekeleza kauri ya hapa Kazi tuu ambayo faida yake wanaiona mpaka sasa , ambapo kila idara ya Serikali inafanya kazi yake ipasavyo tofauti na Vyama vya upinzani hakuna kazi nyingine wanayo ifanya zaidi ya malumbano.

Katika Sherehe za kuadhimisha miaka 40 Wilaya ya Kakonko ilifanya shughuli za Kufanya usafi Wa Zahanati ya Wilaya hiyo, kufungua ujenzi wa Ofisi ya Chama cha Wilaya pamoja na kikao cha Wanachama kilicho husisha upokeaji wa Kadi kutoka kwa Wananchama wapya wa CCM .
mjumbe wa halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kigoma Prof Joyce Ndalichako na baadhi ya wanachama wa chama hicho wakishirika kufanya usafi katika kuadhimisha miaka 40 ya CCM .
Wajumbe na wanachama mbalimbali wa chama CCM katika kuadhimisha miaka 40 ya kuzaliwa kwake,walishiriki kwenye kazi mbalimbali za kijamii ikiwemo ujenzi na kufanya usafi
Baadhi ya ya wanachama wapya 102 kutoka chama cha Act Wazalendo na Chama cha Wananchi Cuf wakila kiapo.

No comments: