Vodacom yazindua simu mpya ya Smart Bomba
· Matumizi yake yapo kwenye lugha ya Kiswahili
· Inauzwa ikiwa imeunganishwa na kifurushi cha intanenti chenye GB 30 za buree kwa miezi 3!
Dar es Salaam,Jumatano Februari 03,2017:Sasa ni wakati wa watanzania kufurahia ubunifu wa kiteknolojia wa mawasiliano unaoendana sambamba na mazingira yao halisi na kufurahia kupata taarifa na burudani kwa njia ya interneti ambapo kuanzia leo wateja wa Vodacom,mtandao unaoongoza nchini wataweza kujipatia simu za kisasa zinazotumia interneti aina ya Smart Bomba.
Simu za Smart Bomba ambazo zimezinduliwa rasmi nchini leo zinapatikana kwa gharama nafuu ya shilingi 99,000/-muundo wa matumizi yake uko katika lugha ya taifa ya Kiswahili pia zinanunuliwa zikiwa tayari zimeunganishwa na kifurushi cha interneti chenye GB 10 za buree kwa mwezi na ofa hii inatolewa katika kipindi cha miezi 3 mfululizo kwa ajili ya kumuwezesha mteja kupata na kufurahia intanenti yenye kasi kubwa ya Vodacom mahali popote na wakati wowote.
Mbali na muundo wa matumizi ya simu hii kuwa katika lugha ya Kiswahili na kwendana na mazingira halisi ya maisha ya watanzania walio wengi,simu za Smart Bomba zina umbo la kuvutia,nyepesi na zina kioo cha mbele,cha ukubwa wa kutosha,zinafanya kazi kwa kutumia teknolojia ya android inaongeza kasi ya kuperuzi internet,inayo kamera ya kurekodi na kupiga picha kwa kiwango chenye ubora wa hali ya juu vilevile inao mfumo wa utambuzi wa ramani ya maeneo mbalimbali ujulikanao kama GPS ambao unatoa maelekezo kuonyesha mahali mtu alipo na mahali aendapo kwa urahisi hususani madereva wa teksi ambao huwapeleka wateja wao sehemu mbalimbali wasiozijua,na zimeunganishwa na program za simu za kurahisisha Maisha za Vodacom kama vile M-Paper.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa simu hii,Mkuu wa Masoko wa Vodacom Tanzania kanda ya Dar es Salaam,Domician Mkama,alisema wakati ni huu wa kila mtanzania kuweza kufurahia matumizi ya simu za kisasa zinazotumia internet (Smart Phones) kwa ajili ya kupata taarifa na burudani kutoka mitandaoni kutokana na kupatikana kwa mara ya kwanza kwa gharama nafuu nchini.
“Kuingia sokoni kwa simu za Smart Bomba za gharama nafuu na zilizotengenezwa kwendana sambamba na mazingira na Maisha ya watanzania walio wengi zikiwa zimeunganishwa na GB 30 kwa matumizi ya miezi 3 ya mwanzoni ni ofa ya kipekee ambayo imebuniwa kubadilisha maisha ya wateja wetu walio wengi na kuendelea kuyafanya kuwa murua”.
Mkama aliongeza kusema “Hivi sasa tuko katika zama za kidigitali ambayo mawasiliano ya watu wengi yanafanyika kupitia mitandao ya kijamii ,hivyo wananchi wengi wakiwa na simu za kisasa zinazotumia internet wanaweza kufanya mambo mengi kwa urahisi na haraka kuanzua kwenye biashara,kupata taarifa mbalimbali,kutumiana salamu na kupata burudani za muziki na sinema kutoka mitandaoni”.Alisema.
Alisema wakati ni huu kwa makundi mbalimbali ya watanzania katika jamii kuchangamkia fursa hii pekee kwa kununua simu ya Smart Bomba kwa gharama nafuu na kuwa mtu wa kisasa anayeenda na wakati na simu hizi zinatukuwa zinapatikana kwenye maduka yote yanayouza simu nchini na zina waranti ya mwaka mmoja.
Kwa kutambua kuwa kundi kubwa kwenye jamii linahitaji matumizi ya intanenti kupata burudani na kupakua muziki hususani muziki wa Bongo Flava,uzinduzi wa simu hii na matangazo yake yamemuhusisha mwanamuzi nguli wa Bongo Fleva nchini, Diamond Platnumz.
Akiongea wakati wa uzinduzi huo,Diamond Platnumz aliwapongeza Vodacom kwa kuingiza sokoni simu ya kisasa ya Smart Bomba ambayo imelenga kutumiwa na wananchi wengi kwa kuwa ina unafuu na inaendana na Maisha halisi ya watanzania. “Sasa ni wakati wa kila mtanzania kwenda kidigitali kwa ku chart,kupata nyimbo za wazipendazo live kupitia simu zao na kupakua filamu wazipendazo ,kutumiana salamu na picha kwa njia ya simu,kuperuzi internet na kupata taarifa na burudani kupitia ncha za vidole vyao na haya yote yanapatikana katika mtandao mkubwa nchini wa Vodacom pekee.
Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,kanda ya Dar es Salaam, Domician Mkama(kushoto) akimshuhudia Balozi wa kampuni hiyo,Mwanamuziki nguli wa kimataifa,Nasibu Abdul” Diamond Platinumz” akiongea na wakazi wa Kariakoo jiji la Dar es Salaam leo na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa simu mpya aina ya Smart Bomba yenye matumizi ya lugha ya Kiswahili inayopatikana kwa shilingi 99,000/-tu iliyoambatanishwa na kifurushi chenye intanenti ya GB 10 za buree kwa kipindi cha miezi 3.
Balozi wa Vodacom Tanzania,Mwanamuziki nguli wa kimataifa,Nasibu Abdul” Diamond Platinumz” akiongea na wakazi wa Kariakoo jiji la Dar es Salaam leo wakati wa Uzinduzi wa simu mpya aina ya Smart Bomba yenye matumizi ya lugha ya Kiswahili inayopatikana kwa shilingi 99,000/-tu iliyoambatanishwa na kifurushi cha intanenti chenye GB 10 za buree kwa kipindi cha miezi 3. Kulia ni Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Vodacom Tanzania,kanda ya Dar es Salaam, Domician Mkama.
Balozi wa Vodacom Tanzania,Mwanamuziki nguli wa kimataifa,Nasibu Abdul” Diamond Platinumz” akiwaburudisha wakazi wa Kariakoo jiji la Dar es Salaam leo wakati wa Uzinduzi wa simu mpya aina ya Smart Bomba yenye matumizi ya lugha ya Kiswahili inayopatikana kwa shilingi 99,000/-tu iliyoambatanishwa na kifurushi cha intanenti chenye GB 10 za buree kwa kipindi cha miezi 3.
No comments:
Post a Comment