Dotto Mwaibale, Kisarawe
HALMASHAURI
ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani imetenga Kata 10 kwa ajili ya kilimo
cha mkataba kitakachoendeshwa na Taasisi ya Winamwanga Cultural
Heritage Association.
Mratibu
wa mradi huo kutoka taasisi hiyo, Saidi Simkonda akizungumza juzi
katika uzinduzi wa mafunzo ya kilimo hai na mafunzo ya ufugaji wa kuku
chotara na mafunzo ya utunzaji wa mazingira kwa kutumia vikundi vya
ufugaji wa nyuki yaliyofanyika wilayani humo juzi alisema mradi huo
umelenga kuwainua kiuchumi wananchi wa Kisarawe na Mkoa wa Pwani
kiujumla.
Alisema
taasisi hiyo imepanga kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa ili kuinua
uchumi wa wananchi kupitia vikundi vya ujasiriamali wa kilimo hai na
ufugaji wa kuku chotara pamoja na kuwawezesha kupata fursa za mikopo
katika asasi za kifedha zilizopo wilayani humo.
"Taasisi
yetu imejipanga kuanzisha kilimo cha mkataba ambapo mazao
yatakayopatikana itayanunua na tayari serikali ya Kijiji cha Kuluwi
imetoa ghala la kuhifadhia mazao hayo.
Mgeni
rasmi katika uzinduzi wa mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi wa
Halmshauri hiyo ambaye ni Ofisa Maendeleo ya Jamii, Wanchoke Chinchibera
alisema mradi huo utawasaidia wananchi na kuwa halmashauri ya Wilaya ya
Kisarawe imetenga kata kadhaa kwa ajili ya mradi huo ambazo ni Maluwi,
Vikumburu, Kuluwi na Mafizi.
Alisema
kwa sababu mradi huo ni mpya katika wilaya yao na utafanya shughuli
zake kwa kilimo cha mkataba aliishauri taasisi hiyo kujenga ushirikiano
mkubwa na wananchi kupitia vikundi ambavyo tayari vimesajili na majina
yake kuwepo katika daftari ofisini kwa mkurugenzi wa halmshauri hiyo.
Mgeni
rasmi katika uzinduzi wa mradi wa kilimo cha mkataba kupitia Taasisi ya
Winamwanga Cultural Heritage Association kwa niaba ya Mkurugenzi wa
Halmshauri ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, ambaye ni Ofisa Maendeleo
ya Jamii, Wanchoke Chinchibera akihutubia wadau wa kilimo wa wilaya
hiyo wakati wa semina ya siku moja iliyohusu kilimo cha mkataba
iliyofanyika juzi wilayani humo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa mradi
huo, Mwajuma Motto, Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa wilaya hiyo, Elliot
Mwasabwite na Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi hiyo, Esabela Luoga.
Semina ikiendelea.
Meza kuu.
Mmoja
wa maofisa wa Taasisi hiyo, Wilson Kibugu akitoa maelezo kwa wadau wa
kilimo wa wilaya hiyo wakati wa semina hiyo ya siku moja iliyofanyika
ukumbi wa mikutano wa Wilaya hiyo.
Ofisa Utawala wa Taasisi hiyo, Fatma Shaib (kushoto), akisoma lisala.
Mgeni rasmi Wanchoke Chinchibera akipokea lisala kutoka kwa Ofisa Utawala wa Taasisi hiyo, Fatma Shaib.
Mratibu
Mradi wa Kilimo wa Taasisi ya Winamwnga Cultural Heritage Association,
Saidi Simkonda (katikati), akitoa mada katika uzinduzi wa mafunzo ya
kilimo hai na mafunzo ya ufugaji wa kuku chotara na mafunzo ya utunzaji
wa mazingira yaliyofanyika wilayani Kisarawe mkoani Pwani juzi.
Ofisa
Mauzo wa Kampuni ya Syngeta Tanzania Limited, John Ngoma akielezea
ubora wa mbegu aina ya Sy 514 inayosambazwa na kampuni hiyo kupitia
miradi ya kilimo ya taasisi hiyo.
Mkurugenzi
wa Mradi wa kilimo wa Taasisi ya Winamwnga Cultural Heritage
Association, Mwajuma Motto (katikati), akizungumza katika uzinduzi wa
mafunzo ya kilimo hai na mafunzo ya ufugaji wa kuku chotara na mafunzo
ya utunzaji wa mazingira kwa kutumia vikundi vya ufugaji wa nyuki
yaliyofanyika wilayani Kisarawe mkoani Pwani jana. Kulia ni Mwezeshaji,
Filbert Luoga na kushoto ni mratibu wa miradi wa taasisi hiyo, Saidi
Simkonda.
Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa wilaya hiyo, Elliot Mwasabwite akichangia jambo kwenye semina hiyo.
No comments:
Post a Comment