Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale akifafanua jambo wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange) utakaotekelezwa na kampuni M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao wakisaini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao (Katikati) wakisaini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange).Kushoto ni Meneja Mradi wa ujenzi huo Li Haiquan.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) Jiang Yigao wakibadilisha hati za mikataba mara baada ya kusaini ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange).
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale akitoa maelezo wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara za juu eneo la ubungo (Interchange) utakaotekelezwa na kampuni M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC).
Baadhi ya wawakilishi wa Mkandarasi wa kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) wakifuatilia hafla ya utiaji saini ya ujenzi wa Ubungo interchange Jijin Dar es salaam. Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), leo umetiliana saini na kampuni ya M/S China Civil Engeneering Construction Cooperation kutoka China (CCECC) mkataba wa ujenzi wa barabara za Juu ‘Interchange’ katika makutano ya barabara ya Sam Najoma na Mandela Ubungo jijini Dar es salaam.
Mkataba huo unamtaka Mkandarasi kampuni ya CCECC kutoka China kuanza ujenzi huo mara moja na ujenzi huo unatarajiwa kutumia takriban miezi 30 hadi kukamilika kwake.
Akizungumza mara baada ya kusaini mkataba huo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Eng. Patrick Mfugale amesema zaidi ya shilingi Bilioni 177.4 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo utakaowekewa jiwe la msingi mwezi machi mwaka huu.
“Hakikisheni mnaanza ujenzi mara moja kwani Serikali imeshakamilisha taratibu zote na tayari kiasi cha shilingi bilioni 2.1 kimelipwa kwa ajili ya fidia kwa wananchi walioguswa na mradi huo”. Amesema Eng. Mfugale.
Ujenzi wa Ubungo interchange unajengwa kwa fedha ya mkopo kutoka Benki ya Dunia ambapo Serikali kwa upande wake imeshalipa fidia ya zaidi ya shilingi bilioni 2.1
“Zaidi ya magari 65,000 yanapita kila siku katika katika makutano ya barabara za morogoro,Mandela na sam nujoma eneo la Ubungo hali inayosababisha msongamano katika barabara ya Morogoro ambayo ndio lango kuu la kuingia jijini Dar es salaam hivyo ufanisi wa mradi huo utahuisha hali ya usafirishaji katika jiji la Dar es salaam na kuchochea ukuaji wa uchumi” amesisitiza Eng. Mfugale.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya CCECC Bw, Jiang Yigao amemhakikishia Eng. Mfugale kuwa wataanza maandalizi ya ujenzi huo mara moja na watafanya kazi hiyo kwa wakati.
Imetolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment