Sunday, February 5, 2017

TRUMARK YAWEZESHA VIJANA KWA SEMINA ENDELEVU JIJINI DAR ES SALAAM

Na Zainab Nyamka, 
Globu ya Jamii
Kampuni ya Trumark inayofanya mafunzo ya kuboresha ufanisi katika jamii imefanya mafunzo ya kujitoleta kwa kuwapatia Elimu ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi katika Chuo cha Ustawi wa Jamii Cha Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa TruMark Bi Agnes Mgongo ambaye pia ni Balozi wa Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi Duniani kupitia Umoja wa Mataifa alisema kuwa ni muhimu vijana kutafuta na kukamata fursa mbalimbali kutoka kwenye jamii yao. Ikiwa ni pamoja na kujitolea kupitia vipaji vyao husuani elimu ili kuweza kuitumikia jamii.
Warsha hii iliyolenga kutimiza moja ya majukumu ya kuwa Balozi wa Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi iliambatana na kutoa shuhuda mbalimbali za mafanikio, elimu na ajira huku wakiwajengea wanafunzi wa chuo hicho uwezo wa kutumia fursa mbalimbali zinazowazunguka katika jamii yao.
Mafunzo haya yalihimiza nguvu na matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii. Bi Agnes aliongeza kwa kusema kuwa mitandao ya kijamii ni mizuri hasa unapoamua ikuletee mafanikio katika maisha.
Jukwaa la Kimataifa la Kuwawezesha Wanawake Kiuchumi lina washiriki kutoka nchi 198, watazamaji 900,000, washiriki 18,500 na mabalozi 410 duniani kote.
Bi Agnes aliwashukuru Kampuni ya Kisima kwa kuweza kutambua umuhimu wakuwapatia vijana fursa nakuwezesha kufanikisha warsha hii muhimu. Na shukrani nyingine alizielekeza kwa uongozi wa chuo cha Ustawi wa Jamii cha Dar es Salaam kwa kuruhusu kutumia chuo cha kama jukwaa la kuwapatia elimu hii muhimu wanafunzi wa chuo hicho.
Tunategemea kufikia vijana wengi zaidi ili nao waweze kuwa mabalozi wazuri wa kuwawezesha wanawake kiuchumi hususan kwa nchi yetu ya Tanzania.
 Mkurugenzi wa TruMark Bi Agnes Mgongo  akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Ustawi wa Jamii wakati wa semina ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.

Muwezeshaji na Balozi wa Vijana kutoka East Community Youth Ambassador Platform Kamala Dickson akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Ustawi wa Jamii wakati wa semina ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.
Afisa habari wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Stella Vuzo akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Ustawi wa Jamii wakati wa semina ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi.


Wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii wakijiandikisha wakati wa semina ya kuwapatia Elimu ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi katika Chuo cha Ustawi wa Jamii Cha Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa TruMark Bi Agnes Mgongo  akiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wa semina hiyo waliokaa na wanafunzi wa chuo cha ustawi wa Jamii.Picha na Zainab Nyamka.

No comments: