Thursday, February 16, 2017

SOPHIA MJEMA AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA KUKAGUA VIPIMO NA MIZANI FEKI, ILALA LEO


Mkuu wa wilaya ya Ilala, kwa kushirikiana na Wakala wa vipimo Tanzania (WMA), mkoa wa Ilala, amefanya ziara ya kustukiza katika maeneo mbalimbali, katika kampeni yake ya kudhibiti vipimo na mizani 'feki'. Pichani, Mjema akikagua mzani kwenye bucha moja eneo la Kariakoo, Dar es  Salaam, akiwa katika ziara hiyo, Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo na kulia ni mfanyakazi katika bucha hiyo, Omar Khalfan.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kulia) na Katibu Tawala wa wilaya hiyo Edward Mpogolo (kushoto) wakiwa katika Ofisi ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA), mkoa huo wa Ilala, baada ya kuwasili kwa ajii ya kuanza ziara ya kustukiza kukagua vipimo na mizani feki, katika maeneo mbalimbali leo. Aliyesimamani mwenyeji wao, Kaimu Meneje wa WMA mkoa huo wa Ilala, Alban Kihulla.

Kaimu Meneja wa WMA mkoa wa Ilala, Alban Kihulla, akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kulia), jinsi ya kutofauisha mizani 'feki' na ile iliyo bora, kabla ya kuendelea na ziara nje ya ofisi hiyo
Mjema akionyeshwamizani malimbali feki na iliyo bora, katika karakana ya WMA mkoa wa Ilala

Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza na wapokea mizigo hasa ya viazi mviringo, katika mitaa ya Kariakoo, Dar es Salaam, kuhusu umuhimu wa akuepuka kupokea magunia yaliyojazwa kwa mtindo wa Lumbesa, kwa kuwa utaratibu huo unakiuka vipimo halisi na hivyo kutia serikali hasara kwa kuwa siyo kipimo halali

Mjema akiwafafanulia zaidi kuhusu hasara ya Lumbesa

Mfanyakzi katika Bucha moja eneo la Kariakoo, Omar Khalfan akitoa maelezo kuhusu mzani anaotumia kupimia nyama wateja,katika bucha hiyo. 
Mfanyakzi katika Bucha moja eneo la Kariakoo, Omar Khalfan akitoa maelezo kuhusu mzani anaotumia kupimia nyama wateja,katika bucha hiyo. 
Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (kushoto) na Mkuu wa Wilaya hiyo Sophia Mjema wakimsikiliza kwa makini mfanyakazi wa bucha hiyo 
Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akimhoji mfanyakazi huyo ikiwa kweli ana uhakika mzani wake ni halali 
Ofisa wa MWA (kulia) akijaribu kutumia vipimo vyake, kubaini kama mzani uliokuwa ukitumia katika Bucha ya Ndevu Complete, Kariakoo, siyo feki. Baadaye ulibainika kuwa mzani huo unafaa 
Mfanyakazi wa Bucha hiyo ya Ndevu Complete akiweka nyama kuonyesha mzani unavyopima 
Mjema akizungumza na wananchi na waandishi wa habari baada ya kumaliza sehemu ya ukaguzi wake wa vipimo na mizani, leo. Wapili kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo. (Picha zote na Bashir Nkoromo). 

No comments: