Thursday, February 2, 2017

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Serikali imewahakikishia watanzania kuwa hakuna uhaba wa sukari utakao tokea nchini na itahakikisha sukari inayozalishwa nchini itatosheleza soko la ndani. https://youtu.be/rOqZSR0C-7E

SIMU.TV: Watu watano wanaodaiwa kuwa maarufu kwa uuzaji wa madawa ya kulevya katika jiji la Dar es Salaam wamekamatwa na jeshi la polisi. https://youtu.be/0r2OwLXUd8Q

SIMU.TV: Shirika la ndege Tanzania ATCL limekanusha taarifa zilizo chapishwa na gazeti moja la siku hapa nchi na kuandika ndege ya ATCL yazua balaa. https://youtu.be/4lRWXoUQ-tQ

SIMU.TV: Wizara ya ardhi nyuma na maendeleo ya makazi imetoa siku 14 kwa kituo cha uwekezaji cha EPZA kulipa shilingi milioni 144 ikiwa ni ucheleweshwaji wa malipo ya kodi ya ardhi. https://youtu.be/IbeIB2NWv6U

SIMU.TV: Mamlaka ya mapato nchini imewaomba wateja wa Kimara mwisho mtaa wa Msikitini jijini Dar es Salaam kuwa wavumilivu kutokana na ufinyu wa maegesho ya magari katika kituo chake. https://youtu.be/rGluvD0dEsY

SIMU.TV: Chama cha ushirika cha ELCT kinachomilikiwa na kanisa la KKKT Dayosisi ya kaskazini kimeiomba serikali kuunga mkono vyama vya ushirika ili wanachama wake waweze kijikwamua kiuchumi. https://youtu.be/1pQZSSltQag

SIMU.TV: Wafanyabiashara waliokuwa wakiidai Uchumi Supermarket baada ya kufungwa mwaka 2015 kutokana na kufilisika wameahidiwa kulipwa madeni yao yanayofikia bilioni 6.2. https://youtu.be/bVlQ6owo9bE

SIMU.TV: Mamlaka ya mapato Tanzania TRA imewatangazia wakazi wa Dar es Salaam ambao hawakuhakiki namba ya mlipa kodi kufika kwenye ofisi zao ili kupata maelekezo zaidi. https://youtu.be/lqWNq-46gVk

SIMU.TV: Benchi la ufundi la timu ya Mamelody Sundown ya nchini Afrika Kusini limeishukuru timu ya Azam Fc kwa kukubali kucheza mchezo wa kirafiki jana usiku. https://youtu.be/62yG5E79AxA

SIMU.TV: Shirikisho la mpira wa miguu la dunia FIFA limeitaka klabu ya Yanga kulipa deni la aliyekua kocha wake Ernest Brants pamoja na faini ya asilimia tano kutokana na kuvunja mkataba wake. https://youtu.be/OfUHhW7K9WE

SIMU.TV: Kamati ya utendaji ya klabu ya Simba imetangaza kumalizika kwa mgogoro wake na baraza la wadhamini wa klabu hiyo uliodumu kwa muda mrefu. https://youtu.be/n6bARZ-kYRg

SIMU.TV: Mchezaji bora wa zamani wa Cameroon Patrick Mbona ameitaka timu ya Ghana kutokuidharau timu ya Cameroon itakayo cheza nayo hatua ya nusu fainali ya kombe la mataifa Afrika. https://youtu.be/Lm7D9jAR52c

No comments: