Thursday, February 9, 2017

RC MTAKA AKABIDHI NG'OMBE KWA FAMILIA YA MD KAYOMBO KWA AJILI YA AROBAINI YA KIFO CHA MZEE KAYOMBO

Na Mathias Canal, Mwanza  
Ikiwa ni siku tatu zimepita tangu Marehemu Mzee Antony Raphael Kayombo kuhifadhiwa katika nyumba yake ya milele (kaburini) Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka amezuru kijijini Misasi, Wilayani Misungwi kwa ajili ya kutoa pole kwa familia ya Mzee huyo.
Rc Mtaka aliyeambatana na Mkewe wamefanya sala ya kumuombea mapumziko mema Mzee Kayombo ikiwa ni ishara ya ukamilifu wake wa haki na kheri hapa Duniani.
Pamoja na mkono wa pole kama mila za kiafrika zinavyoarifu Rc Mtaka pia ameikabidhi familia hiyo Ng'ombe kwa ajili ya Arobaini itakayofanyika kijijini hapo ikiwa ni ishara ya ukamilisho wa Msiba huo (HITMA)).
 "Binafsi naamini katika matendo mema hapa Duniani, Mzee wetu ametutoka ni pigo kwa familia na kwetu sote lakini hakuna namna tuna kila sababu ya kulipokea jambo hili kama jambo la kila mmoja wetu japo halizoeleki" aliongeza RC Mtaka.
Akipokea Ng'ombe huyo na kuzungumza kwa niaba ya familia Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo ambaye ni mjukuu wa marehemu Mzee Kayombo amesema kuwa kwa kuwa safari ya kifo ni ya kila mmoja hivyo familia imepokea kifo hicho kama safari ya mwisho kwa Mzee wao lakini inaendelea kumuombea ili aishi maisha ya amani huko alipo.
MD Kayombo amemshukuru Mkuu huyo wa Mkoa wa Simiyu kwa kufika na kuwasalimu waombolezaji ambao bado wapo kijijini hapo sawia na kumtakia majukumu mema katika utendaji wake ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo kote nchini.
Marehemu Mzee Kayombo aliugua ugonjwa wa kibofu cha mkojo ambao ulianza ghafla tarehe 29/1/2017 na kupelekwa katika hospitali ya Misasi, Baadae hospitali ya Sekou Ture na mwishowe Hospitali ya Bugando ambapo alifanyiwa upasuaji ambapo hata hivyo hali yake iliendelea kudhoofika mpaka mauti ilipomkuta tarehe 4/2/2017 majira ya saa mbili usiku.

MUNGU AILAZE MAHALA PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU MZEE ANTONY RAFAEL KAYOMBO. AMENI 

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kijiji cha Misasi
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (kushoto)
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
 Ng'ombe aiyetolewa na Rc Mtaka kwa ajili ya Arobaini ya Mzee Kayombo
 Mwenyekiti wa Asasi ya Wazalendo na Maendeleo Tanzania (AWAMATA) Chief Mrindoko Babu Mwidadi akisaini kitabu cha wageni ishara ya ushiriki wa asasi hiyo katika msiba wa Mzee Kayombo
 Mazungumzo yamenoga mara baada ya makabidhiano ya Ng'ombe
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe Antony Mtaka (katikati) na Mkewe wakifanya maombi katika kaburi la marehemu Mzee Kayombo, Kulia kwao ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Kayombo ambaye ni mjukuu wa Marehemu Mzee Kayombo
 Rc Antony Mtaka Mtaka
 Rc Mtaka akiwasalimu ndugu wa marehemu Mzee Kayombo mara baada ya kukabidhi Ng'ombe

Rc Mtaka (kulia) akisisitiza jambo, kulia MD Kayombo na katikati ni Mathias Canal Mhariri wa Tovuti ya (www.wazo-huru.blogspot.com) wakisikiliza kwa makini busara za mkuu huyo wa Mkoa wa Simiyu
MD Kayombo akiwa na ndugu na jamaa katika mazungumzo ya jioni

No comments: