Friday, February 10, 2017

RC IRINGA AAGIZA WANAFUNZI WASIORIPOTI SEKONDARI WASAKWE


Na matukiodaima blog
SERIKALI ya Mkoa wa Iringa imeagiza wazazi walioshindwa kupeleka Watoto waliofaulu kujiunga na sekondari wasakwe.
Agizo hilo imetolewa leo na mkuu  wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza wakati wa ziara yake  ya ukaguzi wa vyumba vya madarasa kwenye Shule za sekondari wilaya ya Kilolo.
Alisema kuwa ni wajibu wa watendaji wa vijiji na kata kushirikiana na Walimu wakuu wa Shule pamoja na waratibu Elimu kata  kujua idadi ya Watoto waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kuona wameripoti Shule.
" Nawaagiza watendaji wote kufanya msako wa watoto walioshinda kujiunga na elimu ya sekondari"
Alisema mbali ya Watoto hao kusakwa pia lazima wazazi wabanwe kutokana na kushindwa kutimiza wajibu wao  wa kupeleka Watoto Shule.
Mkuu alisema lengo la serikali ya awamu ya tano  chini ya Rais Dkt John Magufuli ni kuona  kila mtoto anakwenda Shule na ndio sababu ya kufuta ada.
Hivyo alisema kwa mazazi atakayeshindwa kusomesha mtoto anapaswa kuchukuliwa hatua  Kali za kisheria.
Alisema mfano katika Shule ya sekondari Lundamatwe kati ya Watoto waliopaswa kujiunga na sekondari hadi sasa ni Watoto wanne ndio walichelewa kujiunga ila baada ya wazazi kubanwa Watoto
Wawili wameripoti na Watoto wawili wanasakwa na kwa wilaya asilimia 17.89 ya Watoto waliochaguliwa kujiunga sekondari hawajaripoti.
"Naagiza hawa Watoto wawili waliokaa nyumbani watafutwe na waletwe Shule kama suala ni umbali wa Shule basi  waletwe kuishi Hosteli "
Kuhusu maabara mkuu  huyo alisema bado kuna changamoto kubwa ya maabara kutokana na wilaya hiyo kugeuza vyumba vya madarasa kuwa maabara hivyo kupelekea upungufu vya vyumba vya madarasa pamoja na maabara zilizo nyingi kuwa chini ya kiwango.
Masenza alimwagiza mkuu  wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah na uongozi wa halmashauri ya kilolo  kufanya jitihada za ujenzi wa vyumba vya madarasa na maabara bora.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah alisema kuwa kasi  ya kuwabana wazazi wasiopeleka Shule Watoto inaendelea na wametoa muda hadi  machi wazazi wote kupeleka Watoto wao  Shule.
Kwa mujibu wa Afisa Elimu Kilolo Stephen Mrosso jumla ya wanafunzi 3734 ndio walichaguliwa kujiunga na sekondari kati yao wavulana 1658 na wasichana 2076 wanafunzi walioripoti ni 2987 wavulana 1287 na wasichana1693.
Wakati wanafunzi ambao hawajaripoti ni 747 wasichana 383 na wavulana 364 kuwa taarifa zilizopo wanafunzi 82 wakiwemo wavulana 36 na wasichana 46 wamejiunga na Shule nyingine nje ya wilaya ya Kilolo na kufanya jumla ya wanafunzi waliopo Shule kufikia 3069 sawa na asilimia 82.19 hivyo bado asilimia 17.89 kuripoti shule
Mkuu  wa Iringa  Amina  Masenza  akisalimiana na walimu  wa shule ya sekondari  Lundamatwe  Kilolo

Mkuu  wa mkoa wa Iringa  Amina  Masenza  akikagua  vyumba vya madarasa


Mkuu  wa mkoa  wa  Iringa  Amina Masenza  akizungumza na wanafunzi wa  kidato cha  nne katika  shule  ya sekondari  Lundamatwe  wilaya ya  kilolo



Mkuu  wa mkoa  wa Iringa  Amina Masenza akikagua madaftari  ya wanafunzi  shule ya  sekondari  Lundamatwe  wilaya ya  kilolo  wakati wa ziara  yake 






Mkuu  wa mkoa  wa Iringa Amina Masenza akikagua  idadi ya  wanafunzi  walioripoti  kuanza na  kidato  cha kwanza  shule ya  sekondari Lundamatwe  Kilolo  huku wanafuzi hao  wakiwa  wamekaa kwa kubanana  viti  vitatu  wakikaa wanafunzi  wanne



Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo  Asia Abdalah  kushoto  akimsikiliza  mkuu  wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza wakati wa kikao  cha majumuisho wilayani Kilolo.



No comments: