Wednesday, February 8, 2017

MKUU WA MKOA WA MJINI MAGHARIBI ATEMBELEA MAANDALIZI YA TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA

Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar  Simai Mohammed Said akitowa maelezo ya kukamilika kwa maandalizi ya Tamasha hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud alipotembelea Ngome Kongwe kujionea maendeleo ya matayarisho ya Tamasha hilo litakalohudhuriwa na Wasanii wapatao 400 kutoka Zanzibar, Tanzania Bara na Nje ya Tanzania kwa kutowa burudani ya Sanaa yenye ubunifu kwa kutumia Tamaduni za Kiafrika. Hapo ni  Jukwaa la amphitheatre.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayuob Mohammed Mahmoud akiwa na Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Simai Mohammed Said akimtembeza sehemu za kumbi zitakazofanyika kwa Tamasha hilo katika Majengo ya Ngome Kongwe Zanzibar.

Fundi Mkuu wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Hamza Omar Abbas akitowa maelezo ya kukamilisha kwa ufungaji wa Vyombo vya Muziki na Umeme kwa ajili ya matayarisho ya Tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika tarehe 9-2-2017, wiki hii.
Mwenyekiti wa Tamasha la Busara Zanzibar Simai Mohammed Said akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, wakati alipofanya ziara kutembelea na kujionea maandalizi ya Tamaasha hiyo wakiwa katika Jukwaa kubwa litakalotumika kwa Wasanii kutowa burudani wakati wa maonesho mbalimbali ya Tamasha kwa Wasanii.
Fundi Mkuu wa Tamasha la Busara Zanzibar Hamza Omar Abbas akimuonyesha vyombo vya muziki vitakavyowawezesha Wasanii wakati wakiwa jukwaani wakiimba kujisikia wenyewe sauti zao wakati wa show zikiendelea. 

Mwenyekiti wa Sauti za Busara Zanzibar Simai Mohammed Said akimuonesha ratiba ya maonesho yote ya Tamasha hilo Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud.
Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar Simai Mohammed Said akizungumza wakati wa mkutano na wafanyakazi wa Tamasha hilo katika viwanja vya mambo club ngome kongwe kwa ajili ya matayarisho ya Tamasha hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammed Mohamoud akizungumza na wafanyakazi wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar alipofika kutembelea kujionea maandalizi ya Tamasha hilo na kuwataka kuitangaza Zanzibar kwa wageni wanaotembelea kujionea maonesho ya Tamasha hilo la Tamaduni za Kiafrika kuwakutanisha wasanii mbalimbali kutoka katika Nchi za Afrika.
Wafanyakazi wa Tamasha la Sauti za Busara wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe Ayoub Mohammrd Mahmoud akitowa nasaha zake kwa wafanyakazi hao wakati alipofika kutembelea maandalizi ya Tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika keshokutwa Zanzibar tarehe 9-2-2017 

Wafanyakazi wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar wakiwa makini kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud alipofika kutembelea na kujionea maandalizi ya Tamasha hilo kukamilika kwa asilimia mia moja ya maandalizi yake.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Tamasha la Sauti za Busara Zanzibar.

No comments: