Saturday, February 18, 2017

MBUNGE WA SHINYANGA MJINI MHE MASELE ATOA MSIMAMO KUHUSU NJAA

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele (CCM) amefanya mkutano wa hadhara na kusikiliza kero za wananchi katika viwanja vya jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nguzo Nane mjini Shinyanga. 
Mkutano huo ulioanza kwa wananchi kueleza kero zao kwa mbunge umehudhuriwa na mamia ya wakazi wa Shinyanga. 
Miongoni mwa kero zilizotawala mkutano huo ni kero ya bei ya maji kubwa,migogoro ya ardhi,jeshi la polisi kudaiwa kuwaonea waendesha bodaboda kwa kuwachapa viboko na uwepo wa mitaro isiyopitisha maji. 
Tatizo la njaa nalo likachukua nafasi yake huku wananchi wakiomba serikali iwapatie chakula cha bei nafuu kwani sasa kuna mfumuko wa bei za vyakula. 
Akizungumza wakati wa kujibu hoja za wananchi wa Shinyanga,mbunge huyo wa jimbo la Shinyanga mjini,Stephen Masele alisema ni vyema busara ikatumika kwa jeshi la polisi kuhusu ukamataji wa waendesha bodaboda huku akiwasisitiza waendesha bodaboda kuzingatia sharia zausalama barabarani. 
Mbunge huyo pia alisema wananchi wa jimbo la Shinyanga wanakabiliwa na njaa  hivyo kuna kila haja kwa serikali kutoa chakula kwa wananchi
SIKILIZA HAPA CHINI WANANCHI WAKIELEZEA JINSI WANAVYOKABILIWA NA NJAA,NA MAJIBU/MSIMAMO WA MBUNGE WA JIMBO LA SHINYANGA KUHUSU NJAA
TAZAMA PICHA MATUKIO KATIKA PICHA WAKATI WA MKUTANO WA HADHARA MBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI STEPHEN MASELE
Diwani wa kata ya Kambarage mheshimiwa Hassan Mwendapole(CCM) akimkaribisha mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini,mheshimiwa Stephen Masele (CCM),aliyekaa kulia kwake.Wa kwanza kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini,ndugu Charles Sangura
Wakazi wa Shinyanga wakiwa katika mkutano
Diwani wa kata ya Kambarage mheshimiwa Hassan Mwendapole(CCM) akizungumza wakati wa kumkaribisha mheshimiwa Masele
Diwani wa kata ya Kambarage mheshimiwa Hassan Mwendapole(CCM) 
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini,mheshimiwa Stephen Masele akizungumza wakati wa mkutano wa hadhara eneo la Fire/jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nguzo Nane mjini Shinyanga ambapo aliwakaribisha wananchi waeleze kero zinazowakabili
Wakazi wa Shinyanga wakieleza kero zinazowakabili mbele ya mbunge wao
Wananchi wakieleza kero zinazowakabili
Mwananchi akieleza kero yake kwa mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini,mheshimiwa Stephen Masele
Wananchi wakiwa mbele ya mbunge wakitoa kero zao
Mkazi wa Shinyanga mjini,akieleza kwa uchungu kuhusu njaa inayowabili wakazi wa Shinyanga kutokana na bei ya chakula kupanda
Mwananchi akiuliza swali kwa mbunge
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Wananchi wakiwa eneo la mkutano
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini,mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na wakazi wa Shinyanga baada ya kusikiliza kero zao
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini,mheshimiwa Stephen Masele akieleza namna ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi
Wananchi wakimsikiliza mheshimiwa Masele
Wananchi wakimsikiliza Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini,mheshimiwa Stephen Masele
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini,mheshimiwa Stephen Masele akizungumzia kuhusu umuhimu wa kufufua masoko ya Shinyanga ambayo yanazidi kudorora kila kukicha
Wananchi wakiwa eneo la mkutano
Wananchi wakiagana na Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini,mheshimiwa Stephen Masele baada ya kumaliza kuzungumza katika mkutano huo.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

No comments: