MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akimkabidhi mifuko ya saruji kwa ajiri ya ujenzi wa jengo la ofisi ya chama katika kata ya Ruaha kwa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) manispaa ya Iringa Abeid Kiponza
MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa katika eneo la uwanja wa kujenga ofisi ya kata ya Ruaha
MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akibadilishana mawazo na katibu wa ccm manispaa ya Iringa Nuru Ngereja
MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa hama hicho wa kata ya ruaha
MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) manispaa ya Iringa Abeid Kiponza pamoja na viongozi wengine wa chama hicho.
MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati akipokelewa na wanachama wa mtaa wa kigamboni mkoani Iringa
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) ameanza kusaidia Ujenzi wa ofisi za Matawi ya CCM katika kata mbali mbali za Jimbo la Iringa mjini kama sehemu ya majukumu yake ya kukijenga chama hicho ambacho kilipoteza kiti cha ubunge na halmashauri kuchukuliwa na wapinzani.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mifuko ya saruji kwa Ujenzi wa ofisi za Tawi Kigamboni na Ruaha ,Kabati alisema kuwa anafanya hivyo kama njia ya kutekeleza ilani na maadhimio ya miaka arobaini ya chama cha mapinduzi.
“Nakipenda chama changu ndio maana napigana sana kuhakikisha chama cha mapinduzi mkaoni mhapa iringa kinarudi mahala pake na kuhakikisha kinaaminika kwa wananchi na wanachama wa manispaa ya Iringa”.alisema Kabati
Hata hivyo Kabati alisema kuwa ataendelea kusaidia Ujenzi wa ofisi hizo ili kuona ndani ya kipindi kifupi cha miezi mitatu ama sita kila tawi linakuwa na ofisi yake ya tawi na aliwataka wanachama wa CCM kushikamana na kuendelea na Ujenzi wa ofisi hizo pamoja na kujihusisha na shughuli nyingine za kijamii
"Haiwezakani chama kikubwa kama hiki kukosa ofisi za matawi wakati tunamaeneo mengi ya kujenga ofisi nitakikisha tunashirikiana na wanachama na wananchi wengine kujenga hizo ofisi ili kumuunga mkono Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DR John Pombe Magufuli ambaye anapambana kuhakikisha cha mapinduzi kinakuwa chama cha wananchi wa chini na sio matajiri pekee yao".alisema Kabati
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) manispaa ya Iringa Abeid Kiponza aliwataka wanachama kuwa kusahau yaliyopita na kuanza kujenga chama upya.
“Tulipoteza halmashauri ya Iringa na jimbo hivyo inabidi tukae chini na tujipange upya kukijenga chama maana tunajua kwa kujenga ofisi za matawi zitatusaidia kurudisha hadhi na hali ya chama hapa manispaa kwa kutoa huduma bora kwa wananchi wote bila kuchagua chama”.alisema Kiponza
Kiponza alimshukuru mbunge wa viti maalumu Ritta kabati kwa mchango anaoutoa kwa kuleta maendeleo katika manispaa ya Iringa hasa ukiangalia ujenzi wa majengo mbalimbali ya shule,taasisi za kidini,taasisi za kijamii hapa kujenga majengo ya chama.
Lakini Kiponza alimtaka mbunge Kabati kuwasaidia wananchi wanaodhurumiwa na kunyang’anywa mali zao katika manispaa ya Iringa.
“Hapa kigamboni kunawananchi wanapigwa na viongozi wa mtaa kwa kuwa wapo CCM tu na wamenyang’anywa kituo cha kuchotea maji ambacho kilikuwa mradi wa chama cha mapinduzi hivyo lazima upambane kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na mali za chama zinarudi kwenye chama”.alisema Kiponza
Naye Katibu wa CCM manispaa ya Iringa Nuru Ngeleja alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha ofisi zote za chama zinajengwa na zinakuwa katika ubora unaotakiwa kutokana na ukubwa wa chama cha mapinduzi(CCM) na kuahidi kuwa wataendelea kumuunga mkoano Rais wa jamhuri ya muungano ya Tanzania Dr John Pombe Magufuri.
“Sisi tunafanyakazi ya kumsaidia mwenyekiti wetu wa chama ambaye ni Rais wetu kwa kufanya kazi na kuisimamia serikali kufanya kazi kwa uhakika na kuwafaikia na kuwatumikia wananchi waliowaweka madarakani mpaka sasa”. Alisema Ngereja
No comments:
Post a Comment