Saturday, February 25, 2017

BASATA YAOMBA WADAU KUNUNUA SANAA ZA TANZANIA

Kundi la wasanii wa uchoraji la 14+ ikiwa katika maonyesho ya uchoraji picha katika maeneo ya wazi.
Msemaji wa kundi la 14 +, Aman Abeid akitoa maelezo kwa afisa habari wa Barza la Sanaa nchini (BASATA) Agnes Kimwaga wakati wa maonyesho hayo
Mchoraji Nguli wa sanaa za uchoraji, Raza Muhamed akichora wakati wa maonyesho hayo ya uchoraji wa moja kwa moja katika eneo la wazi
Mchoraji Lutengano Mwakisopile akionyesha ufundi wake wa kuchora katika eneo la busatani ya kaburi moja Posta jijini Dar es Salaam
Mchoraji Chilonga Haji akionyesha umahiri wake wa kuchora katika maonyesho hayo



Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Baraza la Sanaa nchini (BASATA) limeziomba tasisi za Serikali na mashirika mbalimbali kuweza kununua kazi za Sanaa za uchoraji za wasanii watanzania na kuacha kununua michoro kutoka nje ambayo aina ubora.

Hayo yamesemwa na Afisa habari wa Basata, Agnes Kimwaga alipotembelea maonyesho ya wazi ya uchoraji wa michoro mbalimbali yaliyoandaliwa na kundi la 14 + la hapa nchini.

“Sanaa za uchoraji na uchongaji za hapa nchini zinatengenezwa katika ubora wa hali ya juu ndio maana michoro mingi inayopelekwa nje kutoka hapa inapata sifa kubwa hivyo ni wakati wa tasisi zetu za umma na ofisi za serikali kuanza kupambwa na michoro hii” amesema Agnes.

Kwa upande wake kiongozi wa kikundi cha 14 +, Lutengano Mwakisopile amewataka watanzania kuendelea kuwaonga mkono katika harakati zao hili waweze kujivunia sanaa hiyo kama ilivyo kwa nchi jirani.
Mchoraji Mins Mims akionyesha ufundi wake wa kuchora katika maonyesho hayo
Mchoraji Caludia Chatanda akitoa maelezo kwa watu waliofika katika maonyesho hayo
Mchoraji wa vibonzo Nathan Mpangala akichora mchoro wake mbele ya wadau katika maonyesho hayo ya wazi
Nathan Mpangala akitoa somo kwa wadau wakifika katika maonyesho hayo
Mchoraji kutoka Vipaji House akionyesha umahiri wake wa kuchora katika maonyesho hayo
wanafunzi wakitazama kwa makini moja ya michoro iliyochorwa na wasanii wa kundi la 14+

No comments: