Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Landanai wilayani Simanjiro wakati aliposimama akitoka Orkesimet kwenda Mererani Februari 16, 2017.
Mwananchi wa kijiji cha Landanai wilayani Simanjiro akiwasilisha kero yake kwa njia ya bango akidai mawasiliano ya simu za mkononi wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliposimama na kuwasalimia wananchi wa kijiji hicho waliokusanyika barabarani. Alikuwa akitoka Orkesimet kwenda Mererani Februari 16, 2017.
Wananchi wa kijiji cha Landanai wilayani Simanjiro wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati aliposimama na kuwasalimia akitoka Orkesimet kwenda Mererani Februari 16, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Mererani mkoani Manyara wakati alipowasili kwenye eneo la mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa mikutano, Februari 16, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa mikutano wa Mererani mkoani Manyara, Februari 16, 2017.
Baadhi ya wananchi Mererani mkoani Manyara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia katika mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa mikutano wa Mererani , Februari 16, 2017.
aziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema wingi wa mabango katika mikutano ya hadhara ya viongozi wakuu ni ishara ya wazi kuwa watendaji wa Halmashauri hawawatembelei wananchi na kutatua kero zao.
Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa mikutano wa Mererani mkoani Manyara Februari 16, 2017, Mheshimiwa Majaliwa alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro na watendaji wake kukusanya mabango yaliyokuwa yakionyeshwa na wananchi kwani mengi ya matatizo yanapaswa kumalizwa na viongozi hao na aliwaagiza kurejea Mererani siku inayofuata ili waitishe mkutano na kujibu bango moja baada ya jingine.
Pichani, watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro wakikusanya mabango hayo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Ndugu Ali Juma baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja mikutano wa Mererani mkoani Manyara Februari 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment