Friday, February 17, 2017

Kongamano la Wanasayansi watafiti lamalizika Jijini Mwanza

Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Bonde la Ziwa Victoria ambaye pia ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi cheti cha shukrani, Bi. Joyce Kasebela baada ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kuwa mmoja wa wadhamini wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria lilimalizika jana jijini Mwanza.

Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi), Dkt Leonard Chamuriho (kushoto) akifuatiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Prof. Faustine Kamuzora na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki wakishiriki Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria lililomalizika jana jijini Mwanza.
Sehemu ya washiriki  kwenye Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria, lililofikia tamati jana jijini Mwanza.
Meneja wa Kiwanja cha ndege cha Jiji la Mwanza, Bi. Esther Madale (kulia) akiwa na Bi. Joyce Kasebele wa Kitengo cha Mazingira cha Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali katika Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria. Kongamano hilo lilifanyika Jijini Mwanza.
Mwakilishi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo wa Jijini Mwanza, Bi. Dorah Michael (kushoto) akipata maelezo mbalimbali kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania (TAA) katika maonesho ya Washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria jana jijini Mwanza.
Bw. Prenanning Pamer mkazi wa Mwanza akipata ufafanuzi wa masuala ya mazingira ndani ya viwanja vya ndege, kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi kwenye maonesho ya washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria, yaliyomalizika jana jijini Mwanza.
ASP Andrew Majaliwa (kulia) akiwa ameshika moja ya vipeperushi vya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), baada ya kupata maelezo kuhusu mazingira kutoka kwa Mhandisi Diana Munubi kwenye maonesho ya washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria, lililomalizika jana jijini Mwanza.

No comments: