Kiwanja
cha ndege cha Dodoma, sasa kinauwezo wa kupokea ndege zenye uwezo wa
kubeba abiria 90, baada ya kurefushwa kwa barabara ya kutua na kuruka
kwa ndege kwa kilometa 2.5.
Ndege ya Shirika la ndege la Tanzania (ATCL), leo ikitua kwenye kiwanja cha ndege cha Dodoma ikitokea mkoani Kigoma.
Mizigo
ya abiria wa ndege ya shirika la ndege Tanzania (ATCL), ikiwa ndani ya
gari la kampuni inayotoa huduma ya mizigo ya National Aviation Services
(NAS), kwenye Kiwanja cha ndege cha Dodoma.
Mkuu
wa Dodoma (kushoto) Mhe. Jordan Rugimbana akielekea kupanda ya ATCL
akiwa ni mmoja wa abiria akitokea kwenye Kiwanja cha ndege cha Dodoma na
kuelekea Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Kulia ni Meneja wa kiwanja hicho, Bw. Julius Mlungwana.
Mkuu
wa mkoa wa Dodoma, Mhe. Jordan Rugimbana (kulia) akiagana na Meneja wa
Kiwanja cha Ndege cha Dodoma, Bw. Julius Mlungwana kabla ya kupanda
ndege ATCL, akielekea Jijini Dar es Salaam, leo.
Wanafunzi
wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Uwela ya kitongoji cha
Kikuyu mkoani Dodoma wakiwa katika ziara ya mafunzo kwenye Kiwanja cha
ndege cha Dodoma, leo.
No comments:
Post a Comment