Friday, February 10, 2017

HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe amekanusha taarifa za kuhusika katika utumiaji au kufanya biashara ya dawa za kulevya. https://youtu.be/WYxTzALynlc

SIMU.TV: Jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam limesema linaendelea kuwashikilia na kuwahoji mfanyabiashara Yusufu Manji na askofu Josephat Gwajima kuhusu tuhuma za kuhusika na dawa za kulevya. https://youtu.be/3TY6_ldOoXQ

SIMU.TV: Jeshi la polisi mkoani Mwanza limefanikiwa kukamata kete 240 za dawa za kulevya aina ya Heroin zikiwa zimehifadhiwa katika vyombo maalumu tayari kuingizwa sokoni. https://youtu.be/jAkihTx3Pns

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa amezitaka kampuni na taasisi za umma zinazo daiwa na kampuni ya simu Tanzania TTCL kuhakikisha zinalipa madeni hayo ifikapo juni 30. https://youtu.be/UMpxwRNCWs0

SIMU.TV: Chuo cha diplomasia Tanzania kimekusudia kuanzisha mpango maalumu wa kutoa elimu katika maeneo yenye migogoro ya ardhi ili kutatua migogoro hiyo. https://youtu.be/BS8UdXW_v_o

SIMU.TV: Wakala wa huduma za misitu TFS wilayani Kalambo umesema utaendelea kuwaondoa watu waliovamia msitu wa kalambo ili kulinda uoto wa asili wa msitu huo. https://youtu.be/qZi4gTQWbVI

SIMU.TV: Mtu mmoja amekutwa amefariki baada ya kugongwa kwa gari katika kata ya Ziba wilayani Igunga na kutelekezwa kando ya barabara. https://youtu.be/PiVwIrAINcU

SIMU.TV: Shirika la viwango nchini TBS limeanza kutoa elimu kwa wafanyabisha juu ya umuhimu wa kuzingatia ubora na viwango wanapoagiza bidhaa nje ya nchi. https://youtu.be/bUCAdYIUxhY

SIMU.TV: Taasisi ya kuendeleza kilimo cha biashara nyanda za juu kusini SAGCOT imesema nafasi ya wakulima kulima kilimo cha biashara ni kubwa endapo watazingatia kanuni za kilimo bora. https://youtu.be/SR48AS6_jC8

SIMU.TV: Wakala wa majengo Tanzania TBA umesema umeshakamilisha ujenzi wa majengo manne ya mabweni ya wanafunzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam. https://youtu.be/IZqU8XAcknY

SIMU.TV: Shirikisho la soka Tanzania TFF limesema zoezi la kuwapima umri wachezaji wa timu ya taifa ya vijana Serengeti boys litafanyika kesho katika hospitali ya taifa ya Muhimbili. https://youtu.be/zpgRTmsFWHk

SIMU.TV: Ligi kuu Tanzania bara inatarajia kuendelea kesho katika viwanja tofauti nchini ambapo Simba wanatashuka uwanjani kucheza na Tanzania prisons ya mkoani Mbeya. https://youtu.be/JKZbRy0tDHw

SIMU.TV: Mtoto mwenye umri wa miaka mitano Bradley Lowery ambaye ni shabiki wa klabu ya Sunderland ametembelewa na wachezaji wa klabu hiyo katika hospitali aliyolazwa akikabiliwa na maradhi ya saratani. https://youtu.be/SnxHSY5HkEQ

No comments: