Thursday, February 16, 2017

DC CHONGOLO ATAKA SERIKALI SIPELEKE CHAKULA CHA NJAA

Na Wankyo Gati,,Arusha

Wananchi wa jamii ya kifugaji hususani vijijini wametakiwa kuacha kulalamika kuna njaa na badala yake watumie mifugo wanayofuga kuuza katika minada na kisha kununua chakula cha kutosha majumbani mwao na kuondoa tafsiri ya kupatiwa chakula na Serikali ili hali wanamifugo.

Pia ameitaka Serikali kutowaletea chakula cha njaa,ambapo jamii kubwa imejijengea tabia ya ya kutoacha chakula cha ziada kwa ajili ya Serikali badala yake kutegem,ea kuwa Serikali ittawaletea chakula cha msaada badala yake wabadili mtazamo na tabia zao za kuweza ziada na kuhifadhi chakula endepo kutakuwa na uhaba wa chakula kam hivi sasa kumekuwa na uhaba wa mvua hali ambayo mazao yamekuwa hayastawi kama awali.

Hata hivyo katika hoja hizo Mkuu wa wilaya ya Longido Daniel Chongolo akatumia nafasi hii kuwataka viongozi wasiwajengee wananchi kuwa kuna njaa na badala yake wawajengee uwezo pindi wanapouza mifugo yao wasitumie fedha zao katika masuala mengine na badala yake wanu nue chakula na kwamba yeye katika wilaya yake haitaji msaada wa chakula kwani wananchi wake si masikini wa kununua chakula.

Mkoa wa Arusha umejaaliwa kuwa na wilaya Zaidi ya sita ambapo wananchi wengi wa vijijini ni wa jamii ya kifugaji ambapo katika kipindi cha hivi karibuni kulizuka mjadala kuwa maeneo ya wilaya za Mkoa huo kuna njaa ambapo serikali imekuwa ikipingana vikali na kauli hizo za wananchi na kuzua mjadala mkubwa kwa wananchi.

Hayo yameelezwa leo na Mkuu nwa wilaya ya londigo Daniel Chongolo katika mkutano ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wa kujadili masuala mbalimbali ya Mkoa ambapo mjadala wa hali ya chakula ulichukua sura tofauti kutokana na mabishano baina ya wadau wa chakula na viongozi juu ya hali ya njaa ambapo wengine wanadai njaa Ipo wengine Hakuna ambapo hali ilikuwa hivi ambapo mkutano huo umehudhuriwa na wakuu wote wa wilaya hizo,makatibu tawala ,wakurugenzi,wabunge wa jimbo na viti maalumu na wataalamu mbalimbali ambapo mkutano huo ulifanyika katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halamashauri ya wilaya ya longido Jumaa Mhina anatoa tafsiri ya njaa ambapo anasema kuwa tatizo la njaa linashindwa kutafsiriwa ni nini maana yake kwani chakula si mahindi peke yake na kwamba kuna vyakula vingine kama vile viazi,ndizi na mihogo navyo ni vyakula.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa ya Arusha amesema kuwa hmaoni hayo yatachukuliwa na kupelekwa kwa katibu tawaola na kufanyiwa kazi ili kupata ufumbuzi wa suala hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Rashidi Taka Hata hivyo jamii imetakiwa kutokuwa na dhana ya chakula cha aina moja na kwamba katika ufanyaji wa kazi za aina mbalimbali kama vile kufuga mifugo ya biashara wawe na desturi ya kununua vyakula ili kuweza kuondokana na uhaba wa chakula katika familia au mtu mmmoja mmoja.

No comments: