Wednesday, January 18, 2017

SIMBA YAKAMATWA SHATI NA MTIMBWA LEO, YATOKA 0-0 UWANJA WA JAMHURI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii Morogoro.

Timu ya Simba imeshindwa kuondoka na ushindi kwenye Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro  baada ya kulazimishwa sare ya kutokufungana na wakata miwa wa Morogoro  mtibwa Sugar mechi iliyochezwa leo.

Baada ya matokeo hayo Simba wanaendelea kusalia kileleni wakiwa na alama 45 akiwa  mebel kwa alama mbili dhidi ya mahasimu wao Yanga wenye alama 43 baada ya mechi yao ya jana kushinda dhidi ya Majimaji Songea.

Baada ya mchezo huu Simba wanakutana na Azam Januari 28 kwenye Uwanja wa Taifa.
Henry Joseph akipambana na mchezaji wa Simba Mwinyi Kazimoto katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
 Kipa wa Mtibwa akiondosha mpira langoni mwake  katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
Wachezaji wakiwa wanasubiri kupigwa kwa mpira langoni mwa Simba.
 Mshambuliaji wa Simba Shiza Kichuya akiwa amemfanyia madhambi Rashidi Mandawa  katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.



 Mshambuliaji wa Simba Juma Luizio akiwa anapambana na beki wa Mtibwa Henry Joseph  katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
 Kiungo wa Mtibwa Ally Shomari akipambana na beki wa Simba Hamad Juma  katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
 Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akiutuliza mpira pembeni mwa mabeki wa Mtibwa  katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.
Kipa wa Simba Daniel Aggey akidaka mpira uliopigwa na Rashid Mandawa wa Mtibwa Sugar  katika mchezo wao wa ligi kuu uliomalizika kwa suluhu ya kutokufungana mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro.Picha zote na Zainab Nyamka.

No comments: