Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza
na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya IPP Media yenye
vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv alipotembelea na
kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo Leo January 17, 2017 Jijini Dar es
Salaam.
Mkurugenzi
wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan
Abass(kushoto) akifafanua jambo kwa uongozi na wafanyakazi wa IPP Media
upande wa Televisheni wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye alipotembelea Kampuni ya IPP Media kwenye vituo
vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv Leo January 17, 2017 Jijini
Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza
mara baada ya kuwasili katika kampuni ya IPP media kwa ajili ziara yake
ya kujionea utendaji kazi wa vituo vilivyo chini ya Kampuni hiyo Leo
January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipata
maelekezo kutoka kwa mmoja ya wafanyakazi wa Ipp Media kuhusuana na
ufanyaji kazi wa vituo vya Televisheni vya ITV, EATV na Capital Tv
alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wa vituo hivyo Leo January 17,
2017 Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia
studio ya kutangazia habari katika kituo cha Televisheni cha ITV
alipofanya ziara kujionea utendaji kazi wa vituo vilivyo chini ya IPP
Media Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Sahara Media kwa upande wa Dar es Salaam Bw. Cyprian Musiba
akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Nape Moses Nnauye alipotembelea Sahara Media kwa upande wa Dar es Salaam
kujionea utendaji wake wa kazi Leo January 17, 2017 Jijini Dar es
Salaam.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza
na uongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Sahara Media
alipotembelea na kujionea utendaji kazi wa vituo chini ya kampuni hiyo
Leo January 17, 2017 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Masuala ya Utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania(TCRA) Frederick Ntobi akifafanua jambo kwa uongozi na
wafanyakazi wa Sahara Media wakati Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipowatembelea Leo January 17, 2017
Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiwa
katika picha ya pamoja na uongozi na wafanyakazi wa Sahara Media kwa
tawi la Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake kwa vituo
vilivyo chini ya kampuni hiyo Leo January 17, 2017 Jijini Dar es
Salaam. Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
Na Raymond Mushumbusi WHUSM.
Serikali
imeahidi kuendelea kushirikiana na vyombo vya habari nchini katika
kutoa habari kwa ajili ya kuhabarisha umma kuhusiana na mambo mbalimbali
yahusuyo Serikali katika kutekeleza majukumu yake.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipotembelea na kujionea utendaji
kazi wa Kampuni ya IPP Media kwenye vituo vya Televisheni vya ITV, EATV
na Capital Tv pamoja na Sahara Media kwa tawi la Dar es Salaam.
Katika
ziara hiyo Mhe. Nape Moses Nnauye amehaidi kuendeleza ushirikiano baina
ya Serikali na vyombo vya habari katika utoaji wa habari ambazo ni
muhimu kwa wananchi kujua zikiwemo hatua ambalimbali zinazochukuliwa na
Serikali katika kutekeleza majukumu yake katika kuwaletea wananchi
maendeleo.
“Niseme
kwa kipindi cha nyuma kumekuwa na urasimu wa utoaji wa taarifa muhimu
kutoka kwetu kuja kwenu vyombo vya habari lakini niwahakikishe kuwa sasa
Serikali imefungua milango kwenu na tuendelee kushirikiana katika
kuhabarisha umma wa watanzania” Alisistizia Mhe. Nnauye.
Kawa
upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) na Msemaji Mkuu wa
Serikali Dkt. Hassan Abass amevihakikishia vyombo vya habari nchini
ushirikiano mzuri katika kupata habari za Serikali kutoka katika vitengo
vyote vya Mawasiliano Serikalini.
Dkt
Abass ameeleza kuwa kwa sasa wako katika mpango wa kuboresha vitengo
vya Mawasiliano serikali ili kuboresha upatikanaji wa habari zinazohusu
Serikali.
“Niwahakikishieni
ndugu zangu wanahabari kuwa suala la upatikanaji wa habari kutoka
Serikali litakuwa si la kusumbuana tena na tunatengeneza mfumo katika
vitengo vyote vya Mawasilaino Serikalini ili iwe rahisi kupata taarifa
kutoka kwetu” alisisitiza Dkt Abass.
Aidha
Mkurugenzi wa ITV/Radio One Bibi. Joyce Mhavile ameishukuru Serikali
kwa kuendelea kushirikiana na Vyombo vya Habari vya binafsi nchini
katika kutoa taarifa kwa umma ambazo zimesaidia kuelimisha, kuburudisha
na kutengenza mazingira ya watu kuamini yale yanayotolewa na vyombo
vyao.
Naye
Mkuu wa Sahara Media kwa upande wa Dar es Salaam Bw. Cyprian Musiba
ameipongeza serikali kwa kuona umuhimu wa vyombo vya habari nchini na
kuahidi kuongeza ushirikiano baina yao na Serikali katika upashanaji
habari.
Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye yupo katika
ziara ya siku sita kutembelea vituo vya Televisheni kujionea utendaji
kazi wa vituo hivyo ikiwa pamoja na changamoto zilizopo ili kupata namna
bora ya kuiendeleza sekta ya habari kwa manufaa ya taifa.
No comments:
Post a Comment