Sunday, January 29, 2017

Mahafali ya 32 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)

SERIKALI iko mbioni kujenga Reli ya Kati kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro yenye kutumia umeme ambayo itakuwa ikisafiri kwa kasi ya Kilomita 160 kwa saa. 
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mnyaa Mbarawa ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya 32 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).
Mhe. Mbarawa amesema kwamba kwa sasa Serikali iko katika hatua za mwisho za kumpata mzabuni atakayejenga reli hiyo kwa kiwango cha Kisasa (Standard Gauge).
“Reli hiyo sio Garimoshi, ni reli itayotumia umeme, kwahiyo kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro tutaweza kwenda kwa saa moja na nusu ambapo ndani ya reli hiyo kutakuwa na huduma nzuri na za kisasa ikiwemo huduma ya intaneti na mambo mengine mengi”, alisema Profesa Mbarawa.
Katika hatua nyingine Mhe. Mbarawa amewapongeza Wahitimu wa kozi mbalimbali kwa bidii zao walizozifanya wakati wa masomo yao kuwataka kutumia hazina kubwa ya elimu waliyoipata chuoni hapo kwa manufaa yao binafsi, ya familia na Taifa kwa ujumla.
“Tunasherehekea mahafali haya ya 32 huku chuo kikiwa kimebadilika na kupiga hatua za haraka katika miaka 42 ya kuwepo kwake tangu kianzishwe mwaka 1975, maendeleo makubwa yameonekana na sisi sote ni mashahidi, na maendeleo haya yasingeonekana bila juhudi za pamoja kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi pamoja na juhudi za Baraza la Uongozi, Uongozi wa Chuo, nyie Wanafunzi, wadau wengine na Watanzania wote kwa ujumla, nachukua fursa hii kuwapongeza sana kwa kazi kubwa mlioifanya”, alisema Profesa Mbarawa.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Mhandisi Profesa Zacharia M.D Mganilwa amesema kuwa, anaishukuru Serikali kwa ushirikiano mkubwa inaoutoa katika chuo hicho tangu kuanzishwa kwake takribani miaka 42 iliyopita ambapo ametaja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana ikiwemo ongezeko la Wahitimu toka 688 katika Mahafali ya 31 hadi kufikia wahitimu 1,118 katika mahafali hayo ya 32 ya chuo hicho.

Ameongeza kuwa, mafaniko mengine yanaonekana katika upande wa elimu ya mafunzo yatolewayo chuoni hapo, kuwa ni chuo pekee kinachotoa mafunzo katika sekta ya usafirishaji na uchukuzi, hivyo kimekuwa kikitoa mafunzo kuanzia ngazi ya watendaji yaani Astashahada na shahada na pia kwa Mameneja.
Amezitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili chuo hicho kuwa ni upatikanaji wa vifaa vya kufundishia ambavyo huendana na mabadiliko ya kiteknolojia na baadhi ya vifaa hivyo ni aghali, vile vile suala la mahitaji ya Wataalam katika nyanja mbalimbali ambapo miundombinu iliyopo imekuwa haitoshelezi idadi ya wanafunzi wanaosoma chuoni hapo.
Awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo hicho, Mhandisi. Profesa Blasius Bavo Nyichomba amesema kuwa, chuo hicho kwa sasa kipo katika mkakati wa kuendelea kutafuta fedha za kununua vitendea kazi kupitia mapato ya ndani pamoja na fedha toka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia.

Katika mafahali hayo yaliyofanyika leo 28 Januari, 2017, jumla ya Wahitimu 1,118 wamehitimu katika kozi mbalimbali za Stashahada ya Uzamili, Shahada, Stashahada na Astashahada zitolewazo na Chuo hicho.

Wahitimu pamoja na Viongozi mbaimbali wakiwa katika maandamano kuelekea viwanja vya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kwa ajili ya kumpokea mgeni rasmi na shughuli ya mahafali kuanza chuoni hapo leo 27/01/2017 jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (katikati) akiwa ameongozana na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Zacharia Mganilwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Blasius Bavomara baada ya kupokelewa na Bendi ya Jeshi la Polisi kuelekea kwenye viwanja vya chuo tayari kwa ajili ya kuanza sherehe ya mahafali ya 32 ya chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) 27/01/2017 jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwahutubia Wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Zacharia Mganilwa akiwahutubia Wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Blasius Bavo Nyichomba akiwahutubia Wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi. Profesa Zacharia Mganilwa wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Wahitimu wa kozi mbalimbali toka chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakisikiliza hotuba za Viongozi mbalimbali wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi wakati wa mahafali ya 32 ya chuo hicho yaliyofanyika leo 27/01/2017 chuoni hapo jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa(aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wahitimu wa kozi mbalimbali toka chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) mara baada ya kuwatunuku Stashahada ya Uzamili, Shahada, Stashahada na Astashahada wahitimu hao leo 27/01/2017 jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Profesa Makame Mbarawa(aliyekaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) pamoja na Wafanyakazi wa chuoni hapo mara baada ya mahafali yaliyofanyika leo 27/01/2017 jijini Dar es Salaam.
 (Picha/Habari na Benedict Liwenga-WHUSM)


No comments: