Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,
Kanda ya Kaskazini.
JESHI la Polisi nchini limetangaza kuwahamisha askari tisa wa vikosi mbalimbali vya jeshi hilo waliopoteza mali zao wakati wa tukio la moto lililoteketeza vyumba tisa vya jengo la ghorofa mbili ambalo ni makazi ya askari.
Mbali na hatua hiyo jeshi hilo pia limetoa kiasi cha Sh Milioni tisa kwa familia za askari hao kwa ajili ya kuanza kununua vitu vidogo yakiwemo mavazi baada ya kutoambulia chochote wakati wa tukio hilo zikiwemo sare za jeshi hilo.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani ametoa kauli hiyo jana kwa niaba ya Mkuu wa jeshi la Polisi ,Inspekta Jenerali,Ernest Mangu wakati akizifariji familia za askari hao pamoja na kutembelea jengo lililoteketea kujionea athari za moto huo uliotokea usiku wa kuamkia juzi.
Akiwasilisha salamu za Pole kwa niaba ya IGP Mangu,Kamishna Marijani alisema jeshi la Polisi litaendelea kutoa msaada kwa askari hao hadi pale maisha yao yatakaporejea huku akivishukuru vikosi vya jeshi la zima moto vya uwanja wa ndege wa KIA,kiwanda cha sukari cha TPC na Halmashauri kwa kazi waliyofanya.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi,Wilbroad Mutafungwa amemwelea kamishna Nsato kuwa thamani ya mali za askari zilizoteketea kwa moto imefikia sh Mil 93.9 huku akiomba wadau kujitokeza kusaidia familia hizo.
Tukio la moto katika jengo hilo lililopo jirani na ofisi za kikosi cha kutuliza ghasia lilitokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa 2:30 usiku ,ukianzia katika chumba kimojawapo cha ghorofa ya pili na kuenea katika vyumba vingine nane wakati huo umeme ukiwa umekatika.
Kufuatia moto huo familia tisa za askari hao zenye jumla ya watu 40, ambao 23 ni watu wazima na 17 ni watoto tayari zimepatiwa malazi ya muda katika chuo cha Polisi Moshi wakati taratibu nyingine za kuwasaidia zikiendelea.
Tayari jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limeunda timu ya wataalamu kutoka katika jeshi hilo wakisaidiana na wale wa kikosi cha zimamoto pamoja na shirika la umeme (TANESCO) kufanya uchunguzi wa matukio ya moto katika jengo hilo.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani akiwasili katika eneo lilipo jengo la ghorofa ambalo ni makazi ya sakari lililoungua moto huku akiongozana na Mwenyeji wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa.
Jengo la ghorof mbili ,makazi ya askari Polisi wa vikosi mbalimbali mjii Moshi liliungua moto sehemu ya juu na kueteketeza vyumba tisa pamoja na mali za asakri waliokuwa wakiishi katika vyumba hivyo..
Kamishna Marijani akiangalia athari iliyotokana na moto katika jengo hilo ulioteketeza vyumba tisa zikiwmo samani za ndani na nguo za familia za askari hao.
Kamishna Marijani akizungumza na CPL Erick Mwantingo mmoja wa askari waliopoteza vitu vyote vya ndani katika tukio hilo la moto.
Kamishna Marijani akita pole kwa PC Maswi ambaye pia amepoteza vitu vyote vya ndani zikiwemo nguo katika tukio la moto lililoteketeza sehemu ya juu ya jengo hilo.
Kamishna Marijani akimfariji CPL,Simba baada ya kutembelea jengo hilo kujionea athari iliyotokana na moto huo.
Kamishna Marinaji akimpa pole SGT Hashim baada ya kupoteza vitu vyote vya ndani pamoja na mavazi kufuatia moto ulioteketeza seheumu ya juu ya jengo hilo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akimuongoza Kamishna Marijani kukagua maeneo mengine ya jengo hilo ambalo linakumbwa na tukio la moto kwa mara ya pili sasa.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi ,Nsato Marijani akisalimiana na baadhi ya viongozi pamoja na wageni waliofika kwa ajili ya kutoa pole kwa asakri waliounguliwa vitu katika jengo hilo.
Waliovalia kiraia ni askari Polisi waliofikwa na janga la kuunguliwa moto vitu vya ndani pamoja na mavazi wakionekana wenye huzuni.
Afisa Mnadhimu daraja la kwanza wa jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Koka Moita akizungumza wakati wa ukaribisho wa Kamishna wa Operesheni na Mafunzo ya Jeshi la Polisi,Nsato Marijani alipotembelea kambi ya polisi mjini Moshi.
Kamnada wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi Mwandamizi Wilbroad Mutafungwa akitoa taarifa juu ya tukio la moto katika jengo la makazi ya askari Polisi.
Mkuu wa Shule ya Polisi Kamandanti Matanga Mbushi akizungumza wakati wa kuzifariji familia za askari waliopoteza vitu vyao katika tukio la moto.
No comments:
Post a Comment