Sunday, January 22, 2017

KIKAO CHA KUTAFUTA SULUHU YA MGOGORO WA PORI TENGEFU LA LOLIONDO CHAENDELEA CHINI YA MKUU WA MKOA WA ARUSHA ,MRISHO GAMBO

Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo ameendelea kuongoza vikao vya kutafuta suluhu ya mgogoro wa Pori Tengefu ambao umechukua muda mrefu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika zaiara yake mwezi desemba mwaka jana alimwagiza Mkuu mkoa kuwakutanisha wadau wote na kupata maoni yao ili kuumaliza kabisa mgogoro huo.


Katika kipindi cha siku saba wajumbe wamekutana na kujadili chanzo na hatua zilizochukuliwa pia wametembelea eneo lilikusudiwa kutengwa kwaajili ya mapito ya wanyama na mazalia ya nyumbu sanjari na kuangalia vyanzo vya maji na miundombinu.


Gambo amesema serikali iko makini kuangalia njia bora za uhifadhi huku wananchi wakiendelea na maisha yao ya ufugaji bila kuathiri sekta ya utalii kwa ujumla huku maslahi ya wawekezaji yakilindwa kwani wana mchango mkubwa katika kusukuma mbele maendeleo ya taifa yanayotokana na kodi wanazolipa.


Taasisi mbalimbali zimewakilishwa zikiwemo Tanapa,NCAA,Tawiri,Asasi za kiraia,Jamii ya wananchi wanaoishi Loliondo na serikali ya mkoa na wilaya.

No comments: