Tuesday, January 10, 2017

HABARI KUTOKA TELEVISHENI LEO


Watu 12 wamekufa na wengine 27 kujeruhiwa baada ya Jahazi walilokuwa wakitumia kusafiria kupata dhoruba na kuzama baharini; https://youtu.be/S_CIXi9K0W4

Mwenyekiti wa kamati ya uongozi CUF Julius Mtatiro amemtuhumu mwenyekiti wa chama hicho Prof Lipumba kukwapua fedha kwenye akaunti ya chama; https://youtu.be/sBNPTmuxm9k

Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego amekanusha taarifa zilizoenea katika mitandao ya kijamii kuwa mkoa huo umekumbwa na baa la njaa; https://youtu.be/K26GCJCjMmw

Rais Dkt John Magufuli anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Simiyu ambapo atakagua miradi kadhaa ya maendeleo; https://youtu.be/P2kqXT7nu2g

Jeshi la polisi kanda maalumu Tarime Rorya limewakamata watu 10 waliohusika kumtandika viboko mwanamke mmoja hadharani; https://youtu.be/60tCExcgw14

Kijana mmoja mkazi wa Yombo jijini Dar Es salaam Mahmudu Said anawaomba watanzania kumsaidia fedha kwa ajili ya matibabu; https://youtu.be/-WYFOhsd-vQ

Serikali imezitaka taasisi za kifedha zilizopo chini yake zinahakikisha wananchi wa chini na wale wa kati wanapatiwa mikopo ili kukua kiuchumi; https://youtu.be/uTMobVt7Q9I

Wafanyabiashara wa soko la muda la Sabasaba wilayani Sumbawanga wameiomba serikali kulifanya soko hilo kuwa soko la muda mrefu; https://youtu.be/7iCn_nHz_xg

Shirika la kuhudumia viwanda vidogo SIDO mkoani Kilimanjaro limezindua mradi wa kusindika mazao ili kuwasaidia wajasiriamali; https://youtu.be/SCopRLXQP7I

Timu ya soka ya Azam imekuwa ya kwanza kutinga hatua ya Fainali ya michuano ya Mapinduzi baada ya kufanikiwa kuifunga Taifa Jang’ombe kwa goli moja; https://youtu.be/pk_4FgBoUsU

Klabu ya soka ya Azam mchana wa leo imemtangaza Aristica Cioaba kuwa kocha wake mkuu kwa kandarasi ya miezi sita; https://youtu.be/0wiEZDQIKio

Ligi kuu soka ya wanawake Tanzania bara inatarajia kuendelea siku ya kesho katika viwanja vya miji tofauti, huu hapa mpangilio wa mechi zote; https://youtu.be/hALvcUdfhoM

Shirikisho la soka duniani FIFA hatimaye limeidhinisha mpango wake wa kuongeza wigo wa timu shiriki kombe la dunia na kufikia 48; https://youtu.be/4RmwOhn7qE0

Watu 12 wamefariki dunia na wengine 20 kujeruhiwa baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kutoka Tanga kwenda Pembe kupinduka. https://youtu.be/nz2e3lzqWD8

Waziri January Mkamba atoa wito kwa wananchi wa Zanzibar kuendelea kushirikiana na serikali kutunza hifadhi ya msitu wa Masingini utakao changia kukuza utalii na uchumi. https://youtu.be/XcHcW1DYfb0

Rais John Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na mjumbe maalum wa Rais wa Nigeria nyumbani kwake mkoani Geita. https://youtu.be/7cVoFw9IRNU

Wizara ya Ardhi yauagiza uongozi wa mkoa wa Iringa kufuata mipaka ya wilaya za Kilolo na Iringa iliyowekwa na serikali mwaka 2000 ili kuondoa mgogoro wa mipaka uliopo. https://youtu.be/C45BlpJ6S7Q

Zaidi ya ngombe elfu 16 wamekufa mkoani Morogoro kufuatia ukame unaoyakabili maeneo mbalimbali hapa nchini. https://youtu.be/2L8j-DGh0VY

Waziri wa ujenzi Prof.Mbarawa amtaka mkandarasi anayejenga jengo la kuongozea ndege kukamilisha kazi hiyo ifikapo mwezi November mwaka huu.https://youtu.be/h_3Nxrc_5rE

Baadhi ya wananchi katika wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu waipongeza serikali kwa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami. https://youtu.be/06bUBT6J9Vk

No comments: