Friday, January 27, 2017

DC KAKONKO KANALI NDAGALA ABAINI MADUDU MPANGO WA KUSAIDIA KAYA MASIKINI (TASAF),WAMO WAHAMIAJI HARAMU


Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

MKUU wa Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma kanal Hosea Ndagala ameitaka mamlaka ya uhamiaji kuharakisha kufanyia Uchunguzi kwa kaya 180 ambazo zilibainika kuwa na baadhi ya wakuuu wa kaya wanadhaniwa kuwa ni wahamiaji haramu walioingizwa kwenye mpango wa kusaidia kaya maskini TASAF kinyume cha sheria.

Pia kanali Ndagala aliwataka Wanufaika na walengwa wa TASAF Kutumia fedha wanazo zipata kuanzisha miradi midogomidogo itakayo wasaidia kutoka katika wimbi kubwa la umasikini, na kuacha kutumia fedha hizo kinyume na utaratibu uliokusudiwa kwa kufanyia mambo ya anasa.

Kauli hiyo alitolewa jana wakati wa ziara yake vijijini ya kutembelea wanufaika wa Mradi huo katika Vijiji vya Nyabibuye na vijiji vya kata ya Nyaronga, ambapo alisema lengo la serikali kuanzisha Mfuko huo ni kusaidia Watanzania wanaoishi katika Mazingira magumu waweze kupata fedha za kuwapeleka Shule watoto, kupata chakula milo mitatu kwa siku na kuboresha afya zao na kuanzisha miradi itakayo wasaidia kujikwamua na umasikini.

Alisema katika uhakiki uliofanyika wa kuhakiki watu wasio stahili kuwemo katika mradi huo, iligundulika kwa Wilaya ya Kakonko kuna baadhi ya kaya 180 zinazo nufaika na mradi huo ambapo baadhi ya wakuu wa kaya hizo mmoja wao ni Raia kutoka Nchi ya Burundi wanao endelea kunufaika na mradi kinyume na utaratibu uliowekwa kwa Wanufaika wa Mradi huo.

Ndagala alisema kuwahudumia wahamiaji haramu kwenye mpango wa TASAF ni kuhujumu uchumi wa serikali , endapo itagundulika Watu hao tunao wadhania sio raia ikithibitishwa na Maafisa wa Uhamiaji Watatakiwa kurudisha fedha zote walizo kwisha kuzichukua na kwa Wale wajumbe wa Kijiji walio shiriki kupitisha majina yao yaingizwe kwenye mradi watatakiwa kuchukuliwa hatua .

"Leo nimepita mimi mwenyewe kujionea Wanufaika wa Mradi wa TASAF na nimebaini mambo machache moja wapo ikiwa wahamiaji haramu kuingizwa kwenye mpango, Wanufaika kutumia fedha kama inavyo takiwa wengi wao wanarumia kunywea pombe na mambo mengine nimekuja kuwahamasisha watumie fedha hizo kwa kuwajenga kiuchumi na kwa wale walio bainika kwenye uhakiki majina tumeyafikisha kwa idara ya uhamiaji waweze kufanya upembuzi yakinifu ilikuweza kubaini uraia wao",alisema Kanali Ndagala.

Sauda Lumala ni Mmoja kati ya Wanufaika alisema kwa upande wake alipo pokea fedha za TASAF alinunua Mbuzi na bata ambapo Mpaka sasa anajumla ya Mbuzi watatu na bata kumi alizo zalisha kupitia miradi ya kusaidia Kaya masikini.

Alisema changamoto wanayo kumbana nayo katika suala zima la kuanzisha miradi baadhi ya Wanawake wengi wakipokea fedha hizo waume zao wanawanyang'anya na kuzifanyia mambo yao binafsi hali inayopelekea kushindwa kutumia fedha hizo kwa shughuli zilizo kusudiwa.

Nae Mratibu wa TASAF Wilaya ya Kakonko, Maria Tarimo alisema mpaka sasa kuna jumla ya wanufaika 7775 katika wilaya ya Kakonko zinanufaika na mpango huo ambao umeleta manufaa makubwa na wengi wao wameanza kufikia malengo yaliyopangwa na wameanzisha miradi endelevu itakayo wasaidia kupambana na umasikini.

Alisema katika uhakiki wa Kuwaondoa watu wasio stahili katika Mpango huo waliobainika ni watu 180 wanaozaniwa kuwa sio Raia ambao wataondolewa kwenye mpango huo na watatakiwa kurudisha fedha walizo kwisha kuzichukua kinyume na utaratibu.
MKUU wa Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma kanal Hosea Ndagala  akisalimiana na mmoja wa wanakijiji cha Nyabibuye,wakati Ndagala alipofanya ziara yake kutembelea wanufaika wa Mradi wa TASAF,katika Vijiji vya Nyabibuye na vijiji vya kata ya Nyaronga
 MKUU wa Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma kanal Hosea Ndagala  akimsikiliza mmoja wa wanakijiji cha Nyabibuye,aliyenufaika na mradi wa Kaya Masikini wa TASAF,wakati  alipofanya ziara yake kutembelea wanufaika wa Mradi wa TASAF,katika Vijiji vya Nyabibuye na vijiji vya kata ya Nyaronga.
 Baadhi ya Wanakijiji cha Nyaronga wakimsikiliza MKUU wa Wilaya ya Kakonko Mkoa wa Kigoma kanal Hosea Ndagala  (hayupo pichani) wakati alipofanya ziara yake kutembelea wanufaika wa Mradi wa TASAF,katika Vijiji vya Nyabibuye na vijiji vya kata ya Nyaronga


No comments: