Monday, January 30, 2017

DC BUHIGWE,KANALI MARCO GAGUTI AWATAKA VIONGOZI WA SERIKALI NGAZI ZOTE KUANZISHA NYUMBA KUMI ZA KIUSALAMA


Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

MKUU wa Wilaya Ya Buhigwe Kanali Marco Gaguti amewataka Viongozi wa Serikali ngazi zote kusimamia ipasavyo zoezi la ulinzi na usalama la kuanzisha Nyumba kumi za kiusalama litakalo saidia kukomesha wahamiaji halamu wanao ingia nchini kinyume na sheria na vitendo vya kiuhalifu vinavyo fanywa na watu wasio na mapenzi mema na Nchi yao.

Rai hiyo aliitoa mapema juzi usiku wakati wa doria ya kukagua zoezi la ulinzi wa Nyumba kumi za kiusalama linaloendelea wilayani humo,ambapo Dc Gaguti alibaini baadhi ya Mabalozi wa Nyumba kumi za kiusalama hawana uelewa juu ya uendeshaji wa zoezi hili,hivyo aliwataka maafisa watendaji pamoja na wenyeviti wa vitongoji kutoa elimu hiyo kama walivyo pewa mafunzo kabla ya zoezi hilo kuanza.

Gaguti alisema lengo la kuanzisha Nyumba kumi za kiusalama ni kuhakikisha Kila balozi wa Nyumba hizo, anafahamu kila nyumba ina wakaazi wangapi Pamoja na kuweka daftari la kumbukumbu na kufahamu wageni wanao ingia na kutoka katika kaya hizo, ilikuhakikisha Wahamiaji halamu wanaiingia nchini kinyume na utaratibu wanakamatwa na na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Alisema kumekuwa na Matukio ya kiuhalifu yaliyo kuwa yakifanywa na Wahamiaji halamu wanaoingia Nchini wakiwa na silaha na kushirikiana na baadhi ya Wananchi wa Wilaya hizi zilizopo Mpakani kufanya unyang'anyi kwa kutumia silaha. Zoezi hili la ulinzi wa Nyumba kumi likifanyika kwa ufanisi litasaidia sana kupunguza vitendo hivyo na kubaini wahamiaji wanaoingia.

Aidha Mkuu huyo aliwaomba Wananchi kuacha tabia ya kuwahifadhi wahamiaji halamu wanao ingia kinyume na utaratibu na atakae gundulika anaishi na muhamiaji hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

" Lengo ni kuhakikisha hakuna Wahamiaji haramu Wanao ingia Wilayani mwetu bila kufuata utaratibu. kumekuwa na matukio ya kiuhalifu Wilayani kwetu yanafanywa na Wahamiaji hao. Nimepita katika vijiji nimeona baadhi  wanafahamu jinsi gani ya kufanya zoezi hilo na wengine hawaelewi. nitoe siku tatu kwa watendaji na wenyeviti wa vijiji na vitongoji kufanya marekebisho ya mspungufu Pamoja na kufanya ukaguzi. mimi pamoja na kamati yangu ya ulinzi na usalama tutakuwa tukipita kwa kushtukiza",alisema Kanali Gaguti.

Nae mwenyekiti wa Kitongoji cha Mgwaga, Joseph Mzegwe alisema yeye kama kuongozi katika kitongoji chake wameendelea kufanya zoezi la ulinzi na wameanzisha zoezi hilo na kila nyumba kumi za kiusalama zina viongozi wao wanao endelea na ulinzi na matokeo wanayaona, kuanzia zoezi hilo lianzishwe amani na utulivu vimeendelea kuwepo katika kitongoji hicho na hakuna tukio lolote baya lililo tokea.

Hata hivyo aliwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa mabalozi wao wanapo hitaji kuwahoji juu ya nyumba zao waseme ukweli ilikuepusha usimbufu na kuhakikisha zoezi hilo linakamilika na linaleta manufaa kwa jamii.
MKUU wa Wilaya Ya Buhigwe Kanali Marco Gaguti akisalimiana na baadhi ya wakazi wa Buhigwe,hivi karibuni alipofanya doria ya kukagua zoezi la ulinzi wa Nyumba kumi za kiusalama linaloendelea wilayani humo mkoani Kigoma


MKUU wa Wilaya Ya Buhigwe Kanali Marco Gaguti akikagua moja ya daftari lililowekwa kwa na balozi wa nyumba kumi kwa ajili ya kuorodhsha majina ya wakazi wa balozi husika,Kanali Gagugti alifanya  doria ya kukagua zoezi la ulinzi wa Nyumba kumi za kiusalama linaloendelea wilayani humo mkoani Kigoma

No comments: