Tuesday, January 31, 2017

BOTI YA MIZIGO NA ABIRIA SITA YADAIWA KUPOTEA ZIWA TANGANYIKA,ILIKUWA IKITOKA KIGOMA KWENDA CONGO.

Na Rhoda Ezekiel Kigoma.

BOTI ya mizigo iliyokuwa ikitokea Kigoma kuelekea Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ya Kalemi, imepotea katika ziwa Tanganyika ikiwa na Watu sita pamoja na Shehena ya vitungu gunia 110, ngano mifuko180 ,Mafuta ya taa dumu 20 na kreti za soda 70  ambayo mpaka sasa haijulikani ilipo.

Akizungumza na Wanahabari Mkoani humo kamanda wa polisi  Mkoa wa Kigoma Fredinandi Mtui alisema Mnamo tarehe 23 januari majira ya saa 16:30 jioni boti iliyotengenezwa  kwa mbao MV.Ngendo ya Buchuma, boti ya mizigo inayo milikiwa na  Mussa Hamisi Mkazi wa ujiji Kigoma Manispaa ,iliondoka  Katika Bandari ya Kibirizi ikiwa na shehena ya vitunguu, Ngano na watu sita kuelekea Congo ambayo mpaka sasa haijafika Congo na haijulikani ilipo.

Mtui alisema mpaka sasa boti hiyo haijulikani ilipo na hakuna chochote kilicho onekana kati ya mizigo wala abiria Waliokuwa wamepanda katika boti hilo, Askali wanamaji wakishirikiana na Chama cha Wamiliki wa maboti Wanaendelea na taratibu za kuitafuta boti hiyo inasemekana imepotelea maji ya Kongo.

Alisema kumekuwa na taarifa zilizo kuwa zikizungumzwa mitaani kwamba  kunamiili imeonekana, taarifa hizo sio za kweli hadi sasa hawajajua kama watu hao watakuwa hai au wamekufa maji, tumewasiliana na Watu waliopembezoni mwa ziwa Tanganyika hawajaona kitu chochote hadi sasa , aliwataka Wananchi kuwa na subira kuweza kutambua kama watakuwa salama au wamekufa.

"baada ya kupata taarifa kuhusu  Boti hiyo iliyokuwa ikielekea Congo kwamba haijafika kwa Muda ulio takiwa,Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Wamiliki wa Maboti walianza jitihada za kuitafuta boti hiyo maeneo ya mwambao mwa ziwa Tanganyika, na hatujapata taarifa yoyote ambapo ingekuwa imezama mizigo iliyo kuwemo katika boti hiyo ingekuwa imeanza kuelea, tumewasiliana na  Mikoa baadhi ambayo ziwa Tanganyika limepita pamoja na Nchi za Burundi na Congo kupitia ubalozi mdogo waweze kutujulisha endapo wataiona boti hiyo",alisema Mtui.

Nao Baadhi ya ndugu wa Wasafiri walio kuwemo katika Boti hiyo wameanza kutandika msiba kuwaombolezea Ndugu zao waliopotea katika Boti hiyo , Hamis Kakolwa ni mmoja kati ya abiria waliokuwa wakisafiri kuelekea Kalemii Congo.

Mgeni Kakolwa ni Mdogo Wa Hamis Kakolwa alisema Ndugu yao aliondoka siku ya tarehe 21 akielekea Kalemi kupeleka biashara zake, baada ya siku mbili kupita walifanya mawasiliano na watu wa Congo kujua kama boti waliokuwa wakisafiria ndugu yao imefika wakaambiwa haijafika ndipo walipoa anza kuwasiliana na Mmiliki wa boti hilo na kubaini kuwa boti hilo lilipotelea ziwani.

Kakolwa alisema baada ya familia yao kuona hakuna mafanikio ya kuipata boti hiyo kwa siku 7 kupita waliamua kuandaa msiba wa kjmuombolezea ndugu yao kwasababu hawana uhakika kama atapona au amekufa.

No comments: