Sunday, January 29, 2017

BENKI YA BIASHARA YA MWALIMU, MCB YATOA SEMINA KWA WASHIRIKI WA KONGAMANO LA KISWAHILI, CHUO CHA KUMBKUMBU YA MWALIMU NYERERE JIJINI DAR ES SALAAM

 Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Anastazia Wambura, akitoa hotuba ya ufunguzi wa chilumbo, (kongamano) la Kiswahili, lililofadhiliwa na benki ya MCB, na kufanyika chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kigamboni jijini Dar es Salaam, Januari 27, 2017.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
BENKI ya Mwalimu, (MCB), imetoa semina kwa walimu na washiriki wa Chilumbo, (Kongamano), la Kiswahili lililofanyika Chuo Cha Mwalimu Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam, Januari 27, 2017.
Katika semina hiyo, maafisa wa MCB walielezea huduma mbalimbali zitolewazo na benki hiyo mpya inayomilikiwa na chama cha walimu nchini, (TTU), ambapo Meneja Mahusiano ya wateja wa benki hiyo, Bw.Charles Shadrack, (pichani juu), alisema, benki hiyo inatoa huduma za kibenki ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo yenye riba nafuu.
“Kwa mfanyakazi wa serikali, anachotakiwa kuja nacho baada ya kufungua akaunti kwenye benki yetu ni Salary sleep ambapo tunatoa mkopo wa hadi shilingi milioni 30.” Alisema.
Alisema, benki hiyo pia imo kwenye kundi la mabenki yanayotumia ATM za umoja hivyo mteja anayo fursa ya kupata huduma za kibenki mahala popote nchini.
Akifungua chilumbo hilo, Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Anastazuia Wambura, amewataka washiriki kukienzi Kiswahili kwani ni lugha inayokua kwa kasi duniani.
“Rais wetu ameonyesha njia, niwape changamoto magwiji wa Kiswahili, jifunzeni kwa bidii ili mkitumie kama ajira kwani soko la walimu wa Kiswahili linapanuka siku hadi siku.” Aisema.


 Wasiriki wakifurahia mada zilizokuwa zikitolewa
 Washiriki wakiwa kwenye ukumbi wa Utamaduni palikofanyika chilumbo
 Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Anastazia Wambura, (kushoto), akipena mikono na Meneja Masoko na Uhusiano wa MCB, Bi. Rahma Ngassa, mara baada ya kutoa hotuba yake
 Meneja Masoko na Uhusiano wa MCB, Rahma Ngassa, Meneja wa Huduma kwa wateja wa benki hiyo, Bi.Flora Mbogo na Meneja Uhusiano wa wateja, Bw.Charles Shadrack, wakiwasikiliza washiriki mbalimbali waliohudhuria chilumbo (kongamano), hilo na wakataka kujua huduma zitolewazo na MCB
 Meneja Uhusiano wa wateja, Bw.Charles Shadrack,(kushoto), akifafanua jambo kwa washiriki hawa waliokuwa na kiu ya kujua huduma zitolewazo na benki hiyo mpya kabisa hapa nchini
 Meneja wa MCB, tawi la Samora katikati ya jiji, Bw.Cassian Clovis, (kushoto), akijadiliana jambo na Meneja Uhusiano wa wateja, Bw.Charles Shadrack, na Afisa Mikopo wa benki hiyo, Bw.Isaya Hagamu, huku chilumbo kikiendelea
 Wimbo wa taifa ukiimbwa
 Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, anayeshughulikia masuala ya Mipango, Fedha na Utawala, Dkt.Magreth Shiwa, akitoa hotuba ya kuwakaribisha wageni
Afisa Mikopo wa benki ya MCB, Bw.Isaya Hagamu, akitoa mada juu ya upatikanaji mikopo kwenye benki hiyo.
 Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Anastazia Wambura, akitoa hotuba
 Baadhi ya washiriki wakisikiliza kwa makini
 Msanii Muhogo mchungu naye alikuwepo kwenye chilumbo (kongamano) la Kiswahili



 Afisa Mikopo wa benki ya MCB, Bw.Isaya Hagamu, (wakwanza kushoto), akitoa maelezo ya shughuli zifanywazo na benki hiyo kwa washiriki hawa waliokuwa na hamu ya kutaka kujua huduma zitolewazo na benki hyo
 Afisa Mikopo wa benki ya MCB, Bw.Isaya Hagamu, akitoa mada juu ya upatikanaji mikopo kwenye benki hiyo.
 Mtunzi maarufu wa vitabu Shafi Adam Shafi naye alikuwepo
 Meneja Masoko na Uhusioano wa MCB, Bi. Rahma Ngassa, (katikati), na Meneja Uhusiano wa wateja, Bw. Charles Shadrack, (kushoto), wakimsikiliza mwenyeji wao Meneja Uhusioano wa Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Bi. Evelyn Mpasha


No comments: