Saturday, January 7, 2017

ANNE MAKINDA AONGOZA WAOMBOLEZAJI MSIBA WA ANNA SENKORO


Picha ya marehemu Anna Senkoro enzi za uhai wake.
 Mwili wa aliyekuwa mgombea wa Urais wa Kwanza Mwanamke mwaka 2005, marehemu Anna Senkoro ukiwasili  leo katika Kanisa la Wninner Chapels International lililopo Banana jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
 Mwili ukiwasili kanisani.
 Humphrey Polepole akitoa salama za Chama na Serikali wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu Anna Senkoro.
 Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ilala, Makongoro Mahanga akitoa salamu za Chama chake wakati wa ibada ya mazishi ya aliyekuwa mgombea wa urais wa kwanza mwanamke katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), akitoa salamu za rambirambi wakati wa ibada ya mazishi ya marehemu, Anna Senkoro.
 Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa mgombea wa Urais wa Kwanza Mwanamke marehemu Anna Senkoro katika Kanisa la Wninner Chapels International jijini Dar es Salaam jana, Marehemu alizikwa katika makaburi ya Kinondoni.
Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania, Anne Makinda akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa aliyekuwa mgombea wa Urais wa Kwanza Mwanamke marehemu Anna Senkoro katika Kanisa la Wninner Chapels International jijini Dar es Salaam jana, Marehemu alizikwa katika makaburi ya Kinondoni. 
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza la marehemu Anna Senkoro.
Kada wa Chadema akitoa heshima za mwisho.
Mwili ukiwasili kanisani.  
 Wafiwa.
 Ndugu wa marehemu.
Spika mstaafu, Anne Makinda na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole.
 Kutoka kulia ni Spika mstaafu, Anne Makinda, Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole na Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Ilala, Makongoro Mahanga.
 Jeneza.
 Wafiwa.
 Wafiwa. 
Poleni sana. 





Dk. Senkoro aliyegombea urais mwaka 2005 kupitia Chama cha TPP –Maendeleo alifariki dunia ghafla Januari 4, mwaka huu wakati akipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu.

Shughuli ya kumuaga Dk. Senkoro ilianzia leo nyumbani kwake, Tabata Segerea, kisha mwili wake ulihamishiwa katika Kanisa la Winners Chapel International, Banana, Ukonga kwa ibada fupi, ambapo viongozi walitoa salamu za rambirambi. 

Mbali na Makinda, viongozi wengine waliohudhuria ni; Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM,  Humphrey Polepole na Mwnyekiti wa Chadema Wilaya ya Ilala, Dk. Makongoro Mahanga.

Akizungumza baada ya ibada hiyo, Makinda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), alisema alipokea kwa mshtuko mkubwa kifo cha rafiki yake na mdogo wake huyo katika siasa.

Alisema Dk. Senkoro alijaribu kuwa rais mwaka 2005, lakini Mungu akamwambia anaweza kuwatumikia wananchi kwa njia nyingine kama alivyofanya.

“Tumemuamini Kristo hivyo hatuwezi kufika kwake bila kulala na Anna amefariki dunia katika Ukristo, swali, jiulize wewe kama ungekuwa Senkoro ungekwenda wapi?” alihoji Makinda.

Alisema familia yake ikae kwa amani na kwamba waamini Anna yuko kwa Mungu amekwenda kutuandalia makao.
Naye Dk. Mahanga akitoa salamu za Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na rafiki yake, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, alisema wamesikitishwa na kifo hicho na kuwapa pole ndugu, jamaa na marafiki walioondokewa na kipenzi chao.

"Sisi kama chama tumempoteza kamanda mwenzetu na mpambanaji toka alipojiunga na chama mwaka juzi Julai, yote ni mapenzi ya Mungu," alisema Dk. Mahanga.
Kwa upande wake, Polepole akitoa salamu kwa niaba ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais John Magufuli pamoja na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana alisema:

"Tuishi maisha mema na yenye kutenda haki kwa sababu Biblia inasema taifa linalotenda haki Mungu uliinua pamoja na kuwa waaminifu kwa uajibikaji na kutenda haki."
Dk. Senkoro wakati wa uhai wake aliwahi kufanya kazi katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Gereza la Ukonga, ameacha watoto watu na wajukuu wawili.

Msemaji wa Taasisi ya JKCI, Maulid Kikondo, alisema mara ya mwisho kabla ya kufikwa na mauti, Dk. Senkoro alifika hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu na kufanyiwa vipimo kadhaa ambavyo madaktari waligundua tatizo lililokuwa likimsumbua.

Alisema jopo la madaktari bingwa wa taasisi hiyo walikuwa na nafasi ya kuokoa maisha ya Senkoro iwapo angekubali kulazwa kwa ajili ya matibabu katika kitengo hicho.
Alisema baada ya vipimo alishauriwa kulazwa kutokana na hali yake, lakini Dk. Senkoro alikataa na kutaka kurudi nyumbani. 

No comments: