Tuesday, December 20, 2016

zowezi la kutoa Elimu kwa abiria pamoja na upimaji ulevi kwa madereva lafanyika Jijini Arusha


Na.Vero Ignatus Arusha.

Mabalozi wa usalama wa usalama barabarani kwa kushirikiana na jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani wamefanya zowezi la kutoa elimu kwa abiria pamoja na madereva huku jeshi la polisi wakiwapima madereva ulevi na kukagua ubora wa magari hayo kabla ya kuanza safari kuelekea mikoani

Zowezi hilo limeongozwa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani SSP Nuru Suleiman na katika stendi kuu ya mabasi yaendendayo mikoani na nchini jirani Jijini Arusha huku zowezi hilo likiwa na lengo la kuelimisha,kukemea na kuripoti mwenendo mzima unaokiuka sheria za usalama barabarani.

Kwa upande wake Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Nuru Suleiman amesema kuwa kampeni hiyo inamafanikio makubwa tangia ianze kwenye wiki ya nenda kwa usalama kwani tangia mwanzoni mwa mwaka 2016 hakuna ajali ya basi iliyotokea na kuleta madhara kwa jamii kwa ujumla.

"Kwakweli tunamshukuru sana Mungu kwani tangia mwaka huu uanze hatujapata ajali ya basi inaonyesha madereva wamepata elimu na wanaitendea kazi na tunawaomba waendelee kuwa makini ili ajali ikiwezekana zisitokee kabisa "alisisitiza kamanda Nuru.Aidha amesema kuwa wamekuwa wakiwapima madereva ulevi na madereva ambao wanakiuka sheria za usalama barabarani na pale wanapogundulika na makosa wapo wengine wanalipishwa faini na wengine wanapelekwa mahakamanikufutiwa leseni na kuzuiliwa kuendesha chombo cha moto kabisa.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa mabalozi wa usalama barabarani Bakari Msangi amesema kuwa lengo kubwa la oparesheni abiria paza sauti ni abiria kutambua wajibu na haki yake awapo ndani ya chombo cha usafiri ikiwemo kutokukaa kimya pale anapomuona dereva anakwenda kinyume na sheria za usalama barabarani,ulevi,kuyapita magari mengine mahali ambapo hapastahili,kutoa lugha zenye utata kwa abiria,dereva kuongea na simu wakati anaendesha,yote haya anatakiwa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi.

Aidha amesema kuwa abiria anatakiwakutoa taarifa pale dereva anapokuwa kwenye mwendo kasi, kufunga mkanda awapo ndani ya gari ili kwamba kama imetokea dharura yeyote asiweze kuhamishwa kwenye kiti alichokaa,pia wawapatie jeshi la polishi ushirikiano kwaajili ya usalama zaidi.

"Unajua abiria wengine ni chanzo cha ajali kwani wanakuwa wanamchochea dereva kuendesha kwa mwendo kasi,wanapoulizwa na askari hawasemi kama kuna tatiuzo hilo ni kosa hebu wapeni ushirikiano jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani ni kwaajili ya faida yenu jamani."alisisitiza Bakari

Naye mwenyekiti wa usalama barabarani Jijini Arusha bi.Stella Rutaguza amesema kuwa kazi kubwa abiria kutokukaa kimya pale anapomuona dereva anakiuka sheria za usalama barabarani ili kuweza kuepuka ajali ambazo zinaepukika.Amesema zowezi hili la Operesheni Abiria Paza Sauti litaendelea hadi April 2017.
Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SSP Nuru Suleiman akiwa katika kituo cha kikuu cha mabasi yaendayo mkoania na nchi jirani ,mkoani Arusha tayari kwa kutoa elimu kwa abiria na madereva leo 19Desemba 2016.Picha pamoja na habari na Vero Ignatus Blog.

Kamanda wa Usalama barabarani akiwa anatoa maelekezo kwa Mabalozi wa usalama barabarani( RSA)Katika stendi kuu ya mabasi yaendayo mikoani na nchi jiarani mkoani Arusha leo 19Desemba2016.Picha na habari na Vero Ignatus Blog.
Mabalozi wa Usalama barabarani( RSA)wakiwa tayari kuanza kazi ya kutoa elimu kwa Abiria namna ya kuutambua wajibu wao na haki zao wakiwa katika chombo cha usafiri.Picha na habari na Vero Ignatus Blog.

Kutoka kushoto ni mwenyekiti wa Usalama barabarani mkoa wa Arusha bi.Stella Ruraguza akizungumza na mwenyekiti wa wakata tiketi stendi kuu ya mabasi yaendayo mkoani na nchi jirani Babuu Jumanne .Picha pamoja na habari na Vero Ignatus Blog
Wa kwanza kushosto ni WP 6905 Neema Tesha pamoja na WP 5048 Coplo Mwajuma wakiwa kazini katika kukagua magari kabla hayajaanza safari kama inavyoonekana pichani nyuma yao kuna basi linaloonekana tayri wameshalikagua.Picha na habari na Vero Ignatus Blog
Wa kwanza kushoto ni koplo Athilio Choga aliyepo katikati ni Vehicle Inspector Koplo Songoi na wa

No comments: