Saturday, December 17, 2016

Wasanii Wa Hip Hop Tz Wamerudisha Ushindani Na Bongo Fleva, Lakini Je, Unafahamu Ukweli Huu?

Tukiwa tumekaribia kufunga mwaka, tumeona wasanii wengi wa rap na Hip Hop wakijitahidi sana na kurelease nyimbo kali na zenye ubora wa hali ya juu kuliko hapo awali. Hapa nazungumzia nyimbo kama Dume Suruali, Muziki na Astara Vaste.
Kuna mijadala mingi inaendelea kuhusu ni nani msanii wa kwanza kufikisha views milioni moja katika YouTube, ila leo mimi ningependa kuongelea contribution ya Azma katika Hip Hop ya Tz. 
Azma Mponda si jina geni kwa watu wote wanaofuatilia historia ya muziki wa kizazi kipya, amekuwa kwenye muziki kwa kipindi kirefu na amefanya mambo mengi.  
Azma ameanza kupenya masikioni mwa watu tangu mwaka 2008 alipoachia nyimbo kama my name is hip hop, bongo fleva inakufa nk.
Aidha Azma alipata kujulikana zaidi mwaka 2008, baada ya kuachia wimbo wa kipimo cha penzi, ambao inasemeka ni wimbo bora wa mapenzi kuwahi kutokea, ukisikiliza hata leo, utahisi ni wimbo mpya kutokana na maudhi yake. Hii imepelekea wasanii wengi kama Belle 9  kumzungumzia Azma kama mwana muziki bora mwenye uwezo wa kuandika nyimbo za mapenzi, na msanii Chindo alidiriki kumfananisha Azma na mwanamuziki LL cool J wa Marekani.
Kwa upande wa wasanii wakongwe kama Profesa Jay na Fid Q  wamewahi kumuelezea AZMA kama msanii bora ambaye hapewi heshima anayostahili. Profesa Jay alimpandisha Azma kwenye show ya Kili music tour mjini Kahama na kutumia zaidi ya dakika tano kumuongelea na kumpa nafasi ya kuimba, Mtangazaji wa Victoria FM Jose fly na mwana habari mkongwe Fredrick Bundala ( sky walker) wamewahi kumzungumzia Azma kuwa miongoni mwa wasanii kumi ambao wanachukuliwa kawaida na wadau wa muziki wakati ana uwezo mkubwa sana 
Hata hivyo umaarufu wa Azma ulianza kuongezeka sana mwaka 2014 na 2015 baada ya kuachia nyimbo kama Kuwa na Azma, Utata wa Katiba nk , Wimbo ulio mfanya Azma akatambulika zaidi ni wimbo wake wa Jinsi ya kumfikisha mpenzi, ambao ulimpa umaarufu sana kwenye mitandao ya kijamii. Wimbo huu ulipelekea Azma kuwa msanii wa kwanza wa Hip Hop kufikisha views Milioni moja You tube… https://www.youtube.com/watch?v=z4_6Xc68UBg .
 Wasanii wengi walifurahi recodi mpya iliyowekwa na Azma, P the MC alikuwa ni msanii wa kwanza kuandika habari ya Azma kuwa msanii wa kwanza kufikisha views 1,000,000 akikanusha uvumi ulianza kuenea kwamba msanii Mr Blue ndiyo wa kwanza.
Nimeshawishika kuandika habari hii ya Azma baada ya kuona waandishi wengi wana andika habari tofauti kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na msanii wa kwanza kufikisha idadi ya hiyo ya watazamaji. Waandishi huwataja wasanii wengine pasipo kumtaja Azma Mponda, wengi tunajiuliza, ni kwa nini msanii mahiri kama huyu anaachwa katika mazungumzo na wakati ukweli unajulikana?
Azma Mponda ameachia wimbo wake mpya wa Astara Vaste akimshirikisha msanii Belle 9, Tazama https://www.youtube.com/watch?v=tUfsubi1qNo , watu wengi katika mitandao ya kijamii na vituo vya redio wanazungumza kuwa, huu ndiyo wimbo bora ukilinganishwa na nyimbo za wasanii wengine nchini, kuanzia kwenye Audio ya wimbo mpaka Video imepelekea watu wengi akiwepo Mwana mziki na Lecturer wa chuo Cha St Augustine, (Kinye) kuandika article kwenye ukurasa wake wa instagram (@thisiskinye) kuwa katika nyimbo zote zilizotoka mwisho wa mwaka huu, wimbo wa Azma ndiyo bora zaidi,
 “kwangu huu ni wimbo bora kati ya tatu kubwa zilizotokea last week… namaanisha wimbo huu ni mkubwa zaidi ya Muziki ya Darassa feat Ben Pol na Dume suruali ya Fa ft Vee @azmamponda na @belle9tz wamefanya kitu kikubwa sana kwenye wimbo huu na kuufanya kuwa wimbo bora kwangu, actually ndio collable nzuri zaidi kuwahi kuisikia ikihusisha hip hop na artist muimbaji”
….. kama haitoshi Kinye alimaliza na maneno yafuatayo   “nakumbuka kuwa main stream haikupi kipaumbele lakini wewe ni msanii wa kwanza wa hip hop kufikisha views 1,000,000.”alisema Kinye
Kutokana na habari hii ningependa kuwaachia watanzania maswali yafuatayo?
1.       Ni kwanini wasanii bora kama Azma Mponda hawa pewi nafasi wanayo stahili kuwa nayo?
2.       Je ni kweli waandishi wanao andika habari hizi hawajui kuhusu historia ya Azma?
3.        Na kama wanajua kwa nini wanapotosha uma?
4.       Na kwa nini wanaandika habari bila kufanya tafiti za kutosha?
5.       Je watanzania wenzangu wenye mapenzi ya kweli na nchi yetu tuna wasaidiaje wasanii kama Azma ?
6.       Ni kweli kwamba hawa watu wachache wanao andika habari zisizo na ukweli wana nguvu kuliko  Uma wa watanzania?
 Astara Vaste lyrics version
Mimi kama Mkenya, na mpenda muziki wa Tanzania, nimekuwa nikifuatilia sana maendeleo ya wasanii mbalimbali na Azma akiwa mmoja wa wasanii tulioweza kuandika article kumhusu, huku Africa mzima wakimkubali kwa comments mbalimbali kwenye mitandao. Kwa hivyo nimeonelea niwapatie the true story about Tanzanian Hip Hop kwa wale wasio na the real facts. Muziki wa Azma unasikilizwa sana huku Nairobi ambapo wapenzi wa Hip Hop wanamkubali sana. Tangu tumjue Azma, amekuwa msanii mwenye bidii kubwa na ameweza kuwainspire wasanii wengi wa Tanzania na Kenya kufanya kazi pamoja mpaka sasa tunaona wengi wakifuatua nyendo zake. Pia, Azma amekuwa msanii anayebadilika na kuonyesha ubunifu wa hali ya juu. Kuna progress kubwa kwenye mziki wake tangu kwenye nyimbo kama Kipimo Cha Penzi, Kuwa Na Azma (ambazo tulizizungumzia katika blog zetu) mpaka sasa kwenye Astara Vaste.
------------------- 
Holly Rahman
Editor, All Around Africa
@AfricaOnMov

No comments: