Monday, December 19, 2016

WAENDESHA PIKIPIKI ZINGATIEA KANUNI ZA BARABARANI NA KUFUATA SHERIA ZA BARABARANI.

 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga  Firbato Sanga akizungumza na vijana wa Umoja wa  endesha piikipiki (Bodaboda) zaidi ya 1580 juu ya kuwataka waendesha Pikipiki hao kuzingatia mafunzo waliyoyapata ikiwamo kufuata sheria za barabarani na kuzingatia sheria za  barabarani na kanuni, katika hafla ya kuwapa vyeti na leseni iliyofanyika  mkoani Pwani. Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.
 Mbunge wa  Jimbo la  Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na vijana wa Umoja wa  waendesha piikipiki (Bodaboda) zaidi ya 1580 na kuwataka kufanya Kazi hiyo Kwa uaminifu mkubwa na zaidi kuona ndio sehemu yao ya ajira kama zilivyo ajira zingine, katika hafla ya kuwapa vyeti na leseni mkoani Pwani.
 Meneja wa Bumaco Insurance Tawi la Gurden Evenue,Tumani Samweli akifafanua jambo mbele ya vijana wa Umoja wa  waendesha piikipiki (Bodaboda) zaidi ya 1580 mkoani Pwani.
 Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Mkuu wa Usalama barabarani Wilaya ya Mkuranga,Hamidu Mtianjola juu ya kufanya Kazi zao kihalali,ambapo aliwapongeza kwakuweza kuhitimu mafunzo hayo ya uendeshaji wa Pikipiki na miongoni mwao kupata leseni.
 Waendesha piikipiki (Bodaboda) Wakichangai damu katika hafla ya kuwapa vyeti na leseni mkoani Pwani.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga  Firbato Sanga akiwa kwenye picha ya pamoja na viongizi wa mbalimbali na  waendesha piikipiki (Bodaboda) zaidi ya 1580 mkoani Pwani.
 Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga  Firbato Sanga akikabidhi leseni kwa mwaendesha piikipiki,Salum Ally Bahari katika hafla ya kuwapa vyeti na leseni iliyofanyika  mkoani Pwani.

No comments: